Lunyungu
JF-Expert Member
- Aug 7, 2006
- 8,873
- 1,906
Jaji Warioba: Hii Ni Hatari
WAZIRI Mkuu mstaafu, Jaji Joseph Warioba amesema amekerwa na tabia ya wanasiasa kupakana matope na kuonya kuwa kisingizio cha utawala bora kisitumiwe kutaka kuangusha dola zilizopo madarakani.
"Tukosoe lakini si kupata maslahi kisiasa naona ndiyo tabia ya sasa kupakana matope kupata maslahi kisiasa. Tusiache kupambana na rushwa, lakini tusipakane matope kwa maslahi ya siasa," Jaji Warioba aliwaambia waandishi wa habari ofisini kwake Oysterbay, Dar es Salaam jana.
Sambamba na hilo, mwanasiasa huyo maarufu nchini alisema ameshitushwa na madai ya ufisadi yaliyoelekezwa kwa baadhi ya viongozi wa serikali, akiwamo Rais Jakaya Kikwete na Rais Mstaafu Benjamin Mkapa."Mengine yanashitusha. Umoja wa nchi hii unaweza kufika mahali pabaya. Yaani Rais anaitwa fisadi kwa sababu hizi na zile tu.
Huyu ni mwanadamu kama wengine, lakini ndiyo symbol (alama) ya Taifa, ukishamwita fisadi na unakwenda unazungumzia hivyo hakuna uongozi wa Taifa."Hata Mkapa aliyemtangulia anaitwa fisadi, hivi hivi tu, habari hizi zinaleta picha gani?
Kwamba alijitajirisha yeye na ndugu zake katika miaka yake 10."Mkapa kama binadamu alikuwa na weakness zake, lakini kwa nchi hii huwezi kufuta historia yake," alisema Jaji Warioba katika mkutano ambao alizungumza kwa makini na kwa busara, huku akitumia mifano mbalimbali kujenga hoja zake mbele ya waandishi waliokuwa kimya wakimsikiliza.
Alisema ameshangazwa na siasa iliyojitokeza katika miaka ya karibuni ya kupakana matope, ndani ya serikali na katika vyama vya siasa, akionya kuwa hiyo itaipeleka nchi pabaya.Lakini zaidi, akawataka viongozi wa serikali, wapinzani na waandishi wa habari, kujiuliza kama kweli habari hizo na mambo yanayoandikwa, ndivyo vipaumbele vya wananchi.
"Rushwa imekuwa silaha ya kisiasa, watu wanatumia good governance (utawala bora) kutaka kuangusha utawala uliopo madarakani."Siku hizi wakubwa wakizungumzia utawala bora, ujue wanazungumzia regime change (mabadiliko ya uongozi).
Nia yao ni kutaka kuondoa utawala ule. Angalia Irak. Sababu ya Marekani ilikuwa kumuondoa Saddam. Simtetei Saddam, lakini nia yao ilikuwa kumuondoa. Leo hii mauaji ni ya kutisha kuliko wakati mwingine wowote."Jana nimemwona Mugabe anazungumza UN.
Wakubwa Zimbabwe wanazungumzia good governance, suluhisho ni Mugabe ang'oke, ardhi si issue, issue ni Mugabe."Good governance inatumiwa kama silaha ya kisiasa, kubadili utawala. Watu wanaamini ukiondoa utawala, rushwa itakoma, Siamini," alisema Jaji huyo aliyewahi kuwa pia Waziri wa Sheria na Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Alisema rushwa nchini imekuwa ikiongezeka kiasi kuwa hata wananchi wa kawaida, sasa wanashiriki kwa kiasi kikubwa, lakini hiyo siyo sababu ya kuondoa utawala."Unataka regime change au kuendeleza utawala. Kwa hiyo, mnawaambia wananchi hawa ndiyo wala rushwa, wakiondoka mambo safi, mimi inanipa taabu.
"Watu wameacha kushughulikia matatizo ya wananchi, mambo ya msingi ya wananchi. Kwa mfano, mwaka jana, tumepata tatizo la chakula na umeme, lakini badala ya kuzungumzia jinsi ya kulikabili mwaka huu, watu wako busy kuzungumzia mambo ya uongozi.
"Wanazungumzia nani fisadi, kutueleza mambo yao ya uongozi. Vipaumbele vyetu vinaanza kupotoshwa. Maendeleo hayawezi kuletwa na viongozi na serikali.
Yataletwa na wananchi, serikali inatunga sera tu na kuzisimamia. Yanayokuja sasa ni lawama tu," alisema na kuongeza:"Vyombo vya habari mtusaidie, utawala bora ni kitu muhimu, lakini watu wanahitaji msaada.
Nimesikiliza Bunge hadi ikafika hoja ya Zitto, watu wanajadili masuala ya uongozi tu. Hoja inazungumzwa mazungumzo hayalengi hoja yenyewe.
Hii concentration ya kulaumiana sijui inawasaidiaje wananchi."Alisema ameiona orodha inayodaiwa kuwa ya mafisadi wanaoitafuna nchi, lakini akasema haina jipya kwa sababu imeshawahi kuandikwa, lakini akasema ina maswali mengi.
"Hii si ilitoka katika miezi miwili mitatu iliyopita. Ilikuwa na wafanyabiashara wakubwa, ikaja nyingine kabla ya hii. Hii ndiyo current (ya sasa) ikipita, sijui itakuja nyingine."Wengine wameisambaza, wanaizungumza wananchi hawana details (maelezo ya kina).
Siyo kitu kipya, imefanywa issue (hoja). Msingi unawezekana upo, lakini ndivyo mambo yanavyopaswa kufanywa? Unatudanganya, unachotusaidia hakionekani. Ukitazama mahakamani hatashinda, lakini politically, amepata umaarufu," alisema Jaji Warioba.
Akizungumzia kuhusishwa kwa Rais Kikwete katika orodha hiyo, Jaji Warioba alisema: "Kwa kweli tu Rais alikuwa Waziri hapo kabla, anahusishwa kwa kusaini mikataba wakati huo".
Kuhusu Rais mstaafu Mkapa, huku akishika tama, Jaji Warioba alisema: "Huyu alikuta mfumko wa bei ukiwa zaidi ya asilimia 30, ameondoka uko chini ya asilimia tano."Amekuta katika huduma ya afya tunategemea vipakiti vya dawa ya misaada kutoka nje, ameondoka hali ya sekta ya afya imeimarika kwa kiwango kikubwa.
Amezikuta shule na vyuo katika hali mbaya, leo kuna mabadiliko makubwa katika elimu. Katika miundombinu, amejenga madaraja na barabara.
"Mawasiliano yamekuwa mazuri. Hata vyombo vyenu vya habari vimeongezeka na mawasiliano ya simu leo unaweza kuzungumza hata ukiwa kijijini. Tumeshausahau uongozi wake."Alisema alifikiri kipaumbele cha viongozi wa serikali na wa upinzani na vyombo vya habari, ingekuwa ni kuhimiza suala kama kilimo ambao huu ndiyo msimu wake, badala ya kukazania kulumbana kuhusu uongozi.
"Jana (juzi) nimemwona Mhita anazungumzia suala la mvua, nilidhani hii ndiyo message (ujumbe) ungesambazwa, lakini wangapi wanamsikiliza. Tukiwaandama viongozi hatupati maendeleo. Jana Karamagi, leo Mgonja, kesho sijui nani anakwenda mahakamani. Tukiendelea hivi sijui ," alisema."Tunavyo-behave sisi inaweza kuwa burudani kwa wananchi, lakini isilete maendeleo. Tuache tabia ya kupakana matope, haitatusukuma mbele.
Tusiache kupambana na rushwa, lakini tusifanye hivyo kwa maslahi ya siasa," alisema.Alisema maisha ya wanaharakati na viongozi wanaopiga kelele juu ya wananchi ni bora kuliko ya wananchi, na kuonya kuwa kumeanza kujengwa tabaka miongoni mwa wanajamii.
"Tubadilike, tuwe na vipaumbele vitakavyosaidia wengi, badala ya maslahi ya wakubwa ambayo hali zao ni nzuri," alisema Jaji Warioba na kueleza kuwa mkutano wake huo na waandishi wa habari haukuwa na shikinizo la mtu ye yote."Kawaida yangu najulikana kwa misimamo yangu.
na serikali wala chama. Nazungumza ninachoamini," alisema Jaji Warioba katika mazungumzo ambayo kwa kiasi kikubwa yalijikita katika kuzungumzia madai yaliyotolewa na wapinzani hivi karibuni kuhusu viongozi yaliyodai wanaitafuna nchi.