kanga
JF-Expert Member
- Jan 13, 2011
- 1,025
- 494
Kwa kipindi kifupi nimeshikwa na wasiwasi na mwenendo wa Tume marekebisho ya Katiba iliyo chini ya Jaji na Waziri Mkuu mstaafu Waryoba.
Kitendo cha kutoa na kuchukua muda mwingi kukusanya mawazo na maoni ya vingozi wastaafu waliwengi zaidi ya miaka 70 siamini kama ni sahihi.
Katiba hii inatoa upendeleo wa wazi kwa wastaafu wa serikali kuu utafikiri katiba inayoandaliwa ni ya viongozi wazee wastaafu ambao wengi ni wa wazee na pengine wamekwisha kula pesheni ya mwenyezi Mungu, kumbuka miaka ya kawaida kuishi ni miaka 70 .
Wananchi na maskini wa nchi hii wengi hawakutoa mawazo yao katika mazingira mazuri,wengine walishurutishwa kutoka mashambani ili wakatoe maoni lakini tume hi ya waryoba kwa viongozi wastaafu inawafuata wazee wengine majumbani mwao , upendeleo huu sioni kama pia usiwe katika kutekelezwa katika maoni yao waliyotoa?.
Waryoba katika ili na kamati yake wameteleza, ni vema muda mwingi wangewapa wazee hawa akina Mwinyi, Kingunge,Malecela, Ben, Kaduma na wengineo wengi kuhamasisha vijana wengi kama wanafunzi, bodaboda, wafugaji na wakulima ambao katiba hii itawahusu kwa kiasi kikubwa na wananchi kwa ujumla kushiriki katika kutoa maoni yao ya ujenzi wa katiba mpya ambao katiba hiyo itawaathiri kwa miaka mingine 50 ijayo.
Chondechonde Mzee Waryoba maoni ya wazee hawa wastaafu wasije wakatulisha kasa , na pengine wao kama viongozi wandamizi wengi wao walikuwa na nafasi kuanza na kufanya mabadiliko stahili lakini wengi pia walikuwa wakipinga mchakato wa mabadiliko ya katiba.
Nina wasiwasi, tunawasiwasi na kubebwa na kupewa zulia jekundu kwa wazee hawa katika mchakato wa katiba mpya, hakuna budi wananchi mawazo yao ya kaheshiwa ipasavyo. Naomba kuwasilisha ndg zangu Watanganyika na Watanzania.