Warioba usiwatishe Watanzania!

katiba mpya chini ya serikali ya ccm??
haikwepeki shinikizo la maoni ya wakubwa yenye maslahi ya wachahe kwenye katiba ...
 


Warioba na Prof.Kabudi kwa nyakati tofauti wameelezea kuwa wakati wanakusanya maoni kulijitokeza mawazo aina nne. kwanza kuna waliotaka serikali moja lakini wachache, kuna waliosema serikali mbili hawa walikuwa wengi, na kundi la tatu walisema serikali tatu lakini muungano wa mkataba, la mwisho kuna waliosema serikali tatu lakini muungano uwepo, hawa walikuwa wengi zaidi ya wote.

Kazi ya tume ilikuwa kukusanya maoni na kupima wengi wanasemaje ungekuwa wewe ungefanyaje????? tusiwe walalamishi
 
Kwanza tulitakiwa tupate referendum kama watu wanataka muungano kama ilivyo sasa kwa scotland wanaotaka kujitenga na UK. Ccm wanajua muungano ukivunyika basi na ccm tasambaratika na kuzaa vyama kumi kidogo.
 

Hapo kwenye red mkuu chabuso mimi nakupinga. Si kweli kwamba hamna asiyetaka muungano, mimi binafsi siupendi na siutaki, hususan huu wa Tanganyika na Zanzibar. Siupendi kwa sababu kadhaa:-
1. Sijui faida zake zaidi ya matusi yanayotoka kwa Wazaznibari kwamba sisi tunawang'ang'ania
2. Hakuna nachokiona na kukiita manufaa kwa kuungana kwetu kijamii kwani matatizo ya kiitikadi yanaonekana wazi
3. Matusi na chuki kati ya Zanzibar na Tanganyika yanaletwa na huu muungano

Kama ukinisaidia kuelewa manufaa ya huu MUUNGANO na MWENGE WA UHURU. Otherwise kwangu nitaendelea kuuona kuwa ni kero kwangu binafsi.
 
Last edited by a moderator:
Sitaki, nakataa na napinga serikali tatu bora Muungano ufe.
 


hapo kwenye nyekundu nimepapenda
 
mambo ya kulazimishwa kula wakati nimeshiba sipendi.
Warioba aache kufanya kazi za chama chake.
 
Ni kweli mwanakijiji, Mzee Warioba anacheza mpira na akiwa referee wakati huo huo.
Spot on folk. Halafu eti maoni yetu ana uhuru wa kuyasikiza au kuyapuuza ila ya kwakwe na aliyemtuma sisi lazima tuwasikize wao.

CHADEMA wakishika dola 2015 waanze tu mchakato mpya wa Katiba. We can do a million better both cost and quality-wise than the current shambles.
 
Ni rahisi kwa watanganyika kupoteza mamlaka yao lakini wazbr ni ngumu na hawato kubali milele.
 
WARIOBA STOP...STOP...STOP tunataka ajitathimini waachie Watanganyika na Waznz waamue
 
wanaotaka kuuokoa muungano ni tume au serikali ya ccm? Wanatuchanganya hawa. Mchicha umekuwa mbuyu...
 
Mzee wa Warioba kafuata mapendekezo ya Chadema serikali tatu.

 

Unaonaje muungano ukaitwa zantania na mamlaka yenu muyasalimishe kwa zanzibr halafu tanganyika muwe jimbo la zantania?
 
Last edited by a moderator:
Umenena sawa mkuu. Warioba anakosea kwa kushinikiza mapendekezo yake. Asijifanye kama yeye ndio mrithi wa nyerere kifikra. Hatuwezi kua na mfumo wa serikali tele kuepa kuvunjika muungano. Hao vibaraka wa kuvunja muungano kwanza washashift position yao ya serikali tatu wanasema nyuma ya pazia hawataki muungano. njia pekee ni kuunda rasimu nyingine ya serikali mbili na kwenda kwenye referundum. Kama kuna upande hawakubali muungano uvunjwe. Hatuwezi kuwa watumwa wa muungano badala ya kuhangaika na maendeleo.
 
Unaonaje muungano ukaitwa zantania na mamlaka yenu muyasalimishe kwa zanzibr halafu tanganyika muwe jimbo la zantania?
What is the difference? Unataka tubadilishe jina la nchi? Kitabadilika nini sasa? Labda tupeleke makao makuu ya nchi huko Zanzibar, ili wageni wanaoitembelea hiyo Zantania walazimike kuvuka bahari. Maana kama ni nchi itakuwa ni ile ile tu, na Zanzibar bado itakuwa ni jimbo katika hiyo nchi ambayo tutakuwa kwa pamoja tumeridhia jina lake.
 
Kwanza kabla ya yote inabidi itambulike muungano ni kwa ajili ya nani? Sasa kama wenzetu hawautaki kwanini tuwalazimishe. Kwa maana halisi hakuna umuhimu wa muungano kama upande mmoja hawajaridhia muungano huo.
 

Wanasema umoja ni nguvu utengano ni udhaifu,.......lakini ukiangalia huu mungano tulionao wa Tanganyika na Zanzibar badala ya kujenga nguvu umeleta udhaifu,umeleta chuki baina ya watu wa pabde mbili ambazo zilikuwa hazipo.

wananchi wameanza kulalamika kuhusu mfumo wa huu mungano kwa muda miaka mingi sasa,lakini kama kawaida ya viongozi wetu kujiona wao wako juu zaidi kuliko wale wanaowatawala ndio sasa imefikia ilivyofikia...maji yameshamwagika.

Na bado wanataka kufanya makosa yale yale,hawataki kuwasikiliza wananchi na ndio maana Warioba kawambia ukweli
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…