Waropokaji wakisimuliwa habari huwa haawataki kujiridhisha kuwa ni kweli au la

Mwanasayansi Kalivubha

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2024
Posts
344
Reaction score
926
WAROPOKAJI HUWA HAWAJUI CHOCHOTE BALI MIHEMKO TU

Hutakiwi kuumizwa na habari za waropokaji na tena ukiweza usipoteze nguvu zako kujibizana nao maana wengi wao huwa wanaongozwa na mihemko tu


Waropokaji hata ukiwakuta kwenye vikao mara nyingi huwa wanataka tu wajulikane kwa kuongea chochote hata kama hawajui ki undani kuhusu wanacho ongea, na hapa utakuta ni wabishi kupitiliza kana kwamba wanajua kwa 100%

Waropokaji huwa ni wavivu wa kutafuta ukweli ila ni wepesi wa kuongea wasiyo na uhakika nayo.

Waropokaji wakisimuliwa habari huwa haawataki kujiridhisha kuwa ni kweli au la bali utawakuta mtaani wakieneza habari hiyo kana kwamba wao ndio shuhuda.

Waropokaji huwa wanawahi kudharauliwa , popote alipo mropokaji wewe fuatllia namna anavyoheshimika kwenye jamii utakuta ni kidogo sana kwa sababu tu hawana siri kwenye mambo yao binafsi na hata wanayoeneza yanakosa uhikika na mwisho wa siku huonekana si lolote.

Mwanasayansi Saul kalivubha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…