Huu ni mpango wa nchi za magharibi tu kuonyesha ulimwengu kuwa "uhalifu" wa kivita duniani ni shughuli ya nchi zingine -- sio wao -- na ambazo wanaziona kama vile hazijastaarabika. Mtu wa kwanza kutolewa warrant na mahakama hiyo angepaswa kuwa Bush kwa kufanya uvamizi Iraq na kusababisha vifo vya watu wasiokuwa na hatia zaidi ya milioni moja na wengine milioni mbili kuhama makazi yao na/au kukimbilia nchi za nje.
Tusisahau kuwa karibu dunia nzima ilipinga uvamizi huo kwani haukuwa na sababu yoyote. Sababu zilizoainishwa na Bush zilikuwa za kupikwa kama vile ilivyokuja kudhihirika baadaye. Kwa nini tunasahau? Kwa hivyo Bush na Blair kimakusudi wakauzunguka Umoja wa Mataifa na kufanya uvamizi.
Mahakama hiyo haikuona yote hayo kwa sababu kulikuwa hakuna taifa miongoni mwa yale yanayoendelea kuweka msukumo kwa mahakama hiyo kutoa warrant kwa Bush na chinjachinja wenzake Tony Blair na Dick Cheney.
Hivi hamushangai hata kidogo kwa nini Marekani haikutia sahihi mkataba ulioanziosha Mahakama hiyo? Ni kweli Marekani ilishiriki (wakati wa Clinton) mchakato wa kuanzisha kwake lakini alipoingia Bush aliutupilia mbali mkataba huo na ilikataa kutia sahihi.Na hapo hapo akatangaza kuwa ole wake nchi yoyote ile itakayomkamata askari au raia yeyote wa Marekani na kumpeleka kwenye Mahakama hiyo. Ilikuwa ni dharau kubwa kwa Dunia iliyokuwa inajaribu kukuomesha vitendo vya kuhalifu wa kivita vinavyofanywa na taila lolote bila kujali hadhi au utajiri wake.
Kumbe kukataa kwa Bush kutia sahihi mkataba wa Mahakama hiyo kulikuwa kwa sababu maalum, kwamba Bush mwenyewe alikuwa anatarajia kufanya uhalifu mkubwa hapa dunuiani tangu wakati wa utawala wa Pol Pot wa Cambodia katika miaka ya 70. Jee Mahakam hiyo ambayo haitambuliwi na Marekani inaweza kweli kutoa waranti kwa Bush? Inaweza, lakini nani ataotao wazo, au msukumo hilo lifanyike? Viongozi wa nchi zet ni dhaifu sana mbele ya mataifa haya makubwa
Inakadiriwa waliokufa Darfur kutokana na uhalifu huo wa Bashir wanafikia laki 3idadi ambayo ni ndogo sana ukilinganisha wale waliokufa Iraq. Tuisisahau kuwa Marekani ina undumila kuwili. Hebu ona: Kule Darfur inawaunga mkono wapiganaji wanaopigana dhidi ya Serikali ya Bashir, na ingependa sana serikali hiyo iangushwe. Lakini kule Chad, nchi inayopakana na hilo jimbo la Darfur, Marekani hiyo hiyo inaiunga mkono serikali ya Chad dhidi ya waasi wao ambao mwaka juzi almanusura waiangushe serikali ya Idris Deby.
Tatizo hapa ni jinsi tunavyopumbazwa na nchi za Magharibi. Chad na eneo la Darfur lina utajiri mkubwa sana wa mafuta ambayo Marekani inayamezea mate. Kule Chad tayari iko serikali muafaka inayokidhi matakwa ya Marekani kuchota mafuta, lakini Sudan si hivyo, kwani ingependa Bashir aangushwe, ije serikali "muafaka" itakayoiuzia Marekani mafuta.