The Phylosopher
JF-Expert Member
- Mar 11, 2015
- 1,968
- 2,957
Kwenye kipindi cha asubuhi ya leo wakati wakipitia magazeti wametumia takribani robo tatu ya muda wote wa kipindi hicho kuelezea kadhia ya kupotea kwa watu katika mazingira yasiyoeleweka huku mamlaka husika zikisalia kimya.
Ukweli ni kwamba ukijaribu kuvaa viatu vya wale waliopotelewa na wapendwa wao au jaribu kufikiria wewe ndio umetekwa na madhila unayopitia kwa kweli ni maumivu yasiyoelezeka.
Nimuombe sasa rais wetu atoke hadharani atoe tamko la kuviagiza vyombo vya ulinzi na usalama vishughulikiwa kazdhia hii inayoleta hofu na mtafaruku kwa raia.
Niombe vyombo vingine vya habari vipaze sauti nchi isinyamazie uvunjifu huu wa haki za binadamu ambao umejengeka kuwa wa kawaida sasa katika taifa letu.
Pia soma

- Kuelekea 2025 - Waziri Mkuu Kassim Majaliwa atoa majibu ya matukio ya kupotea na utekaji watu yanaendelea Nchini
- Freeman Mbowe: Viongozi wa CHADEMA na Watanzania wasio na Vyama wanaoendelea kutekwa na Vyombo vya Usalama vya Nchi yetu
- Tamko la Masauni Waziri wa Mambo ya Ndani kuhusu madai ya kusambaa kwa matukio ya utekaji wa Watoto, asema Nchi ipo salama