Wasafi TV inabidi mkajifunze kwa Clouds TV namna ya kurusha vipindi mubashara

Wasafi TV inabidi mkajifunze kwa Clouds TV namna ya kurusha vipindi mubashara

GIRITA

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2016
Posts
4,432
Reaction score
5,864
Hii media imekuja kwa kasi sana, kweli mmeweza kukamata pakubwa kwenye tasnia ya habari mawasiliano na burudani.

Lakini bado mnasafari ndefu sana kufikia media zilizotangulia, msijione mnaweza kufika 10 kabla ya kuanza 1, ni vema kujifua zaidi kupata maujuzi kabla ya kuanza kufanya mambo ambayo ni makubwa sana kwa uwezo wenu.

Jifunzeni kwa wakongwe waliowatangulia itakuwa bora zaidi kuliko kukurupuka na kutuletea migando migando kwenye runinga zetu

Huku uswahilini watu wamejiandaa kufuatilia kwa hamu shoo ya Rayvan akiamsha amsha nyie mnaleta maziwa mgando mnaboa sana nyie madogo, tangu juzi vipindi vya live kule Arusha mliboa mpaka siku ya jana kwenye shoo yenyewe jukwaani ilikuwa ni utopole mwingi sana.

Tangu kuzaliwa sijaona matangazo ya live yenye ubovu kama ule au wakubwa zenu clouds media wakileta matusi kama yale kwenye FIESTA zao, inabidi mfunge safari mpaka CMG mkaulize wanatumia njia gani na vifaa gani kurusha matangazo mubashara.
wasafi.jpg
 
Tangu kuzaliwa sijaona matangazo ya live yenye ubovu kama ule au wakubwa zenu clouds media wakileta matusi kama yale kwenye fiesta zao,inabidi mfunge safari mpaka CMG mkaulize wanatumia njia gani na vifaa gani kurusha matangazo mubashara.
View attachment 1649064
Wafanyie hisani kuwanunulia hivyo vifaa vya kurushia matangazo sio unakuja kubwabwaja tu hapa
 
Hiv kila siku wasafi media kwani chombo Cha habari kipo Wasafi media pekee yake?

Watu wanaipenda, kutoa maoni ya kukosoa kwa ajili ya kujenga ni njia mojawapo ya kwamba watu wanafatilia hiyo TV.

Nadhani wafanyie kazi maoni ya wateja wao.
 
Sio lazima Kila media ipitie kipindi kigum Kama hizo zingine za mwanzo.
Kwanza kabisa unakashifu na Wala sio kukosoa ,.

Nb;Ngoja team wasafi waje[emoji16][emoji16]
 
Hao unao wasifia inabidi wakajifunze EATV,TBC na Azam sioni utofauti wa clouds ,EFM na Wasafi upande wa live events.

Lile basi tu wa TBC ukiambiwa gharama zake tu unaweza ukakuta zaidi ya 2bilion,ile migari ya Azam mikubwa inafika mpaka 3bilion

Kijana Broadcast equipments pamoja na system zake ni za gharama kishenzi na zinahitaji watu waliokwiva kuziendesha na hizo certificate za equipments za broadcast kuzipata lazima ukapige pepa nje ,Tz hapa center zao za mitihani theory pamoja na lab zake hamna.

Ndio maana shoo za kibongo zinazoruka Clouds,EFM na Wasafi quality zake za hovyo hata watu wanaosimamia hivyo vifaa nao wanaungaunga,bora kidogo Azam nina jamaa zangu naona kuna wazungu wanawapa training mara kwa mara.

Broadcasting industry kwa TZ upande wa Technology bado sana,Azam peke yao ndio wana vifaa vya kisasa,kuliko media yoyote Afrika mashariki na kati.Hapa Tz show zote zina sound mbovu,hawana watu wa Sound Engineering walio specilize wengi ujanja ujanja.
 
Nilipata wasaa wakuangalia Tamasha lao Kama sikosei lilikua Mwanza tumewasha na Tigo

Kulikua nautumbo unaoendelea wakuzimazima Taaa mara kiza mara mwanga ikabidi nibadili channel
 
Back
Top Bottom