Wasafi wamegoma kukatìsha kabisa matangazo kwa ajili ya Didah

Wasafi wamegoma kukatìsha kabisa matangazo kwa ajili ya Didah

MSAGA SUMU

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2015
Posts
6,661
Reaction score
21,656
Japokuwa Mangwea hakuwa mfanyakazi wa Clouds lakini mwamba alipoondoka clouds walijitahidi sana kumuenzi. Ngoma za mwamba zilipigwa siku nzima.

Hapo hatujaongelea mtu kama Ruge, wakina Kibonde na Gardner.

Huku Wasafi chini ya meneja vipindi wao baba Levo wako wako tu. Kuanzia usiku, asbuhi, mchana na jioni vipindi vimeendelea kama kawaida. Sijui boss anaona atapoteza muda.

Hii inaset picha mbaya kwa sìsi wafanyakazi wengine tuliobakia hasahasa sisi watu wa kipindi cha michezo. Siku tukiondoka hamna hata namna yoyote ya maana ya kutukumbuka.

Nimecopy mtandaoni.
 
Inasikitisha sana ,atleast wangesitisha vipindi na kupiga muziki wa maomolezo lakini matangazo ya wadhamini yaendelee kupigwa kama kawaida mpaka siku 3.
 
Duniani umuhimu wako wanauona mama yako baba yako na wanao uliowazaa tu hata mkeo usimuweke huyo hana tofauti na rafiki zako wengine wale ambao siku ukifukiwa ft6 wakilipa kisogo kaburi lako tu wataendelea na story zao za Simba na Yanga.
 
Waislamu hatunaga mambo mengi kwenye msiba ,kifo ni kifo ndio maana tumemsitiri leo,chap chao,maisha yaendelee
 
Inasikitisha sana ,atleast wangesitisha vipindi na kupiga muziki wa maomolezo lakini matangazo ya wadhamini yaendelee kupigwa kama kawaida mpaka siku 3.
At least Leo siku nzima wangepiga taarabu tuu vidole juu hasa za wale alio kuwa akiwakandia... Wapi isha mashuziii??
 
In business wise -ingesomeka hivi waomboleze kwa kupiga nyimbo za uzuni Ila vipindi viendelee.

Nadhani heshima aliyopewa Leo katika mazishi yake ni kubwa Sana .

So donation na duration vikipishana mambo Kama hayo hutokea

Dida alikuwa bora Sana she was not icon .
 
Japokuwa Mangwea hakuwa mfanyakazi wa Clouds lakini mwamba alipoondoka clouds walijitahidi sana kumuenzi. Ngoma za mwamba zilipigwa siku nzima.

Hapo hatujaongelea mtu kama Ruge, wakina Kibonde na Gardner.

Huku Wasafi chini ya meneja vipindi wao baba Levo wako wako tu. Kuanzia usiku, asbuhi, mchana na jioni vipindi vimeendelea kama kawaida. Sijui boss anaona atapoteza muda.

Hii inaset picha mbaya kwa sìsi wafanyakazi wengine tuliobakia hasahasa sisi watu wa kipindi cha michezo. Siku tukiondoka hamna hata namna yoyote ya maana ya kutukumbuka.

Nimecopy mtandaoni.
Acha kazi uwakomoe!
 
Kazini alifariki mtu afu msiba upo Dar hapa hapa, aisee, ratiba ziliendelea kama kawaida ikabidi wabishi tutoroke twende msibani. Tulikua tunasubiria iwe official haijawahi kutokea. Iliishia tangazo WhatsApp tu.
 
Back
Top Bottom