Wasafiri Stand ya Magufuli (Dar es Salaam) kupimwa maambukizi ya Vizuri vya Ebola

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2022
Posts
2,780
Reaction score
6,607
Serikali imeweka kituo maalum cha ufuatiliaji wa ugonjwa wa Ebola kwa abiria wanaotoka mikoa ya mipakani mwa Tanzania na nchi jirani katika kituo kikuu cha mabasi cha Magufuli jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na EATV mratibu wa huduma za maabara kutoka Manispaa ya Ubungo Nalimi Nacharo, amesema kituo hicho kitatumika kuwapima ugonjwa wa Ebola abiria wanaoingia nchini kutokea mikoa ambayo tayari serikali imetangaza kwamba ipo kwenye hatari ya kupata ugonjwa huo.

EBOLA WEB .jpg
Kwa upande wake Meneja wa kituo hicho Isihaka Waziri, amesema tayari wameshawaelimisha madereva wa mabasi yanayotoka katika mikoa hiyo kuhakikisha wanapoingia kituini hapo wasishushe abiria mpaka wafike kwenye kituo cha upimaji Ili waweze kupimwa ugonjwa wa ebola

Nao mawakala wa mabasi kutoka nchi za Uganda ambako ndiko ugonjwa huo upo na wale ambao mabasi yao yanatokea maeneo ya mipakani mwa nchi Faraji Musa na Mohamedi Hassan wamesema hatua hiyo ya serikali itasaidia kuzuia ugonjwa huo usiingie nchini na kushauri kuwekwa kwa vituo kama hivyo kwenye maeneo mengine ya vituo vikuu vya mabasi.

Chanzo: EATV
 
Na walioshuka njiani? Au kuna utaratibu wa kuwa-trace?
 
Hicho kituo kingewekwa kwenye mji wa kwanza kutoka mabasi yanapoanzia kama Kahama, Bukoba,mwanza au nzega, kukiweka mbezi inaweza isiwe na tija abiria wanaanza kushukia mbali
Na watakaopandia mbele ya hiyo miji? Kama dodoma au morogoro.
 
Hicho kituo kingewekwa kwenye mji wa kwanza kutoka mabasi yanapoanzia kama Kahama, Bukoba,mwanza au nzega, kukiweka mbezi inaweza isiwe na tija abiria wanaanza kushukia mbali
Wanafanya ya hovyo, wangeweka mipakani.
 
Hicho kituo kuwekwa hapo Magufuli Terminal ni upuuzi mtupu.

Ni sawa na kupima AFYA mkiwa tayari mshafanya mapenzi bila Kinga.

Ilipaswa vituo hivyo vya afya viwepo mipakani mwa inchi ambazo ndy chimbuko la ugonjwa wa EBOLA.

Sasa mtu kishafika Dar,,ameshakutana na wangapi?

Vipi abiria akitoka inchi Jirani na asiende Dar moja kwa moja,akaamua kushuka na kuunganisha gari chalinze na kuelekea mikoa kama Tanga, Kilimanjaro,Arusha.,
Ni nani atakayetambuwa ?

Hicho kituo kiwepo Kwa ajili ya kupima watu wanaotoka Dar kwenda mikoani.
Na sio wanaoingia Dar.

Sent from my Infinix X624 using JamiiForums mobile app
 
Fact
 
Tafadhali rekebisha kichwa cha habari.. 'Vizuri vya Ebola'
Serikali imeweka kituo maalum cha ufuatiliaji wa ugonjwa wa Ebola kwa abiria wanaotoka mikoa ya mipakani mwa Tanzania na nchi jirani katika kituo kikuu cha mabasi cha Magufuli jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na EATV mratibu wa huduma za maabara kutoka Manispaa ya Ubungo Nalimi Nacharo, amesema kituo hicho kitatumika kuwapima ugonjwa wa Ebola abiria wanaoingia nchini kutokea mikoa ambayo tayari serikali imetangaza kwamba ipo kwenye hatari ya kupata ugonjwa huo.

Kwa upande wake Meneja wa kituo hicho Isihaka Waziri, amesema tayari wameshawaelimisha madereva wa mabasi yanayotoka katika mikoa hiyo kuhakikisha wanapoingia kituini hapo wasishushe abiria mpaka wafike kwenye kituo cha upimaji Ili waweze kupimwa ugonjwa wa ebola

Nao mawakala wa mabasi kutoka nchi za Uganda ambako ndiko ugonjwa huo upo na wale ambao mabasi yao yanatokea maeneo ya mipakani mwa nchi Faraji Musa na Mohamedi Hassan wamesema hatua hiyo ya serikali itasaidia kuzuia ugonjwa huo usiingie nchini na kushauri kuwekwa kwa vituo kama hivyo kwenye maeneo mengine ya vituo vikuu vya mabasi.

Chanzo: EATV
 
Hicho kituo kuwekwa hapo Magufuli Terminal ni upuuzi mtupu.

Ni sawa na kupima AFYA mkiwa tayari mshafanya mapenzi bila Kinga.

Ilipaswa vituo hivyo vya afya viwepo mipakani mwa inchi ambazo ndy chimbuko la ugonjwa wa EBOLA.

Sasa mtu kishafika Dar,,ameshakutana na wangapi?

Vipi abiria akitoka inchi Jirani na asiende Dar moja kwa moja,akaamua kushuka na kuunganisha gari chalinze na kuelekea mikoa kama Tanga, Kilimanjaro,Arusha.,
Ni nani atakayetambuwa ?

Hicho kituo kiwepo Kwa ajili ya kupima watu wanaotoka Dar kwenda mikoani.
Na sio wanaoingia Dar.

Sent from my Infinix X624 using JamiiForums mobile app
Nadhani hujawahi safiri nje ya mipaka ya Tanzania kwa taarifa yako huwezi toka au kuingia nchini bila kupita kitengo cha afya kinaitwa port health kwa kiinglishi.

Hapo utafanyiwa vipimo na ukaguzi wa vyeti vya chanjo mbalimbali.

#MaendeleoHayanaChama
 
Hoja ni; Wamejiandaa vipi kama akipatikana mwenye ugonjwa au mwenye dalili zake hapo kituoni? Watatangaza au wataficha taarifa na kufanya mambo kimya kimya?

Kwasababu kuonekana kwa hilo hema bila taarifa kamili inaweza kuzua hofu kwa baadhi ya wananchi na wageni.

Badala ya kutengana na WHO kama walivyofanya wakati wa JPM na Corona; GoT safari hii ishirikiane nao WHO toka mwanzo ili kama badae mambo yakiharibika dunia isitulaumu.
 
Nadhani hujawahi safiri nje ya mipaka ya Tanzania kwa taarifa yako huwezi toka au kuingia nchini bila kupita kitengo cha afya kinaitwa port health kwa kiinglishi.

Hapo utafanyiwa vipimo na ukaguzi wa vyeti vya chanjo mbalimbali.

#MaendeleoHayanaChama
Unamfundisha samaki kuogelea?

Back
Top Bottom