SoC01 Wasafiri wawili

SoC01 Wasafiri wawili

Stories of Change - 2021 Competition

ihama107

Member
Joined
Jul 22, 2021
Posts
6
Reaction score
3
WASAFIRI WAWILI_Moment(2).jpg

ISMAIL MAYUMBA




Watu wawili wakiwa wameianza safari ya baharini, wakiwa kwenye jahazi na safari yao ikigharimu miaka yao tisa katika kuishi. Sio kama awali bali saivi bahari ina machafuko na vimbunga vya kila aina na mawimbi yanayotisha. Ikafika kipindi wakaanza kusikia njaa na kwa bahati nzuri kwenye jahazi kulikuwa kuna mti wenye matunda tisa. Mti ukanena haya maneno

Kama mlivyoniona nina matunda tisa na kila moja litatumika kwa mmoja. Sharti ni kwamba mmoja achukue tunda na mwengine achukue mbegu'

Bila ya kufikiria, msafiri mroho akachukua tunda na kumtupia mbegu msafiri mstamihimilivu. Msafiri mstamihilivu akachukua mbegu na kuipanda kwenye jahazi. Hiyo hali ikawa inaendelea kila mwaka na kila msafiri akiwa na hoja yake.

Msafiri mroho
'Kwa hakika bahari ni chafu na ina vitimbi vya kila aina kwa hivyo bora niyanufaishe matamanio na kupata starehe mbalimbali kwani muda wowote jahazi linaweza kupinduliwa '

Msafiri msatamihilivu
'Ninafanya hivi kwa sababu nawekeza katika maisha yangu ili nije kunufaika baadae na kama tabu za njaa na kukesha macho muda mrefu basi nipo tayari kukabiliana nazo kwani siwezi kuendekeza starehe za muda mfupi kuharibu maisha yangu yote'

Jahazi likasonga kwa miaka tisa na kufikia tamati ya safari yake. Wakashuka kwenye jahazi, msafiri mroho akaanza kusikia njaa na kumuona msafiri mstamihilivu akiwa mwenye kushiba na kustareheka sana. Kumbe msafiri mstamihilivu alikuwa anapanda mbegu na zile mbegu zikawa zinakua na kushamri kuwa miti na kila mti ukitoa matunda kedekede na mwisho wa safari akawa na matunda ambayo yanaweza kumlisha mpaka mwisho wa uhai wake na yakabakia.

UFUMBUZI
JAHAZI-MAISHA
MTI-ELIMU
BAHARI-DUNIA

MAEMBE-NGAZI ZA ELIMU

Msafiri mroho alikuwa sahihi kiasi kwa hoja yake kwamba bahari ni chafu akimaanisha vifo ni vingi siku hizi na kinakukuta katika umri wowote kutokana na majanga na vita mbalimbali. Akaamua kutimiza hamu zake na kuchezea elimu. Hoja hiyo haina mashiko kwani anayejua maisha ya mwanadamu na kifo chake ni Mungu na hakupaswa kuendekeza starehe na hata hivyo starehe zilikuwa za muda mfupi . Msafiri mstamiilivu alinufaika na juhudi zake pamoja na kuvumilia kwake kipindi cha elimu. Matunda anayoyapata ni mafanikio yale aliyoyatengeneza kipindi anasoma

MWANDISHI- ISMAIL MAUMBA
MAWASILIANO- 0624000455
 
Upvote 2
Na imani mtasoma kazi yangu ya uandishi na kunipigia kura niweze kushinda 🤲🙏
 
Back
Top Bottom