Wasafirishaji mnafanyaje hii biashara??

Ndio maana sijapigia siku 365 mkuu. Lengo ni kuweka hizo unforeseen events zote.
 
Huu ni mwandiko wa mtu mzima mwenye akili zake
 
Just imagine milioni 700+ afu unapakia abiria 50 kwa elfu 50 Dar Kahama, unalipa wafanyakazi, engine kubwa inanyonya mafuta kama walevi wa KASKAZINI.

Bado ukodi ofisi, trafiki, Latra etc!!
Mnapigaje hapo???View attachment 2854877
50×50=milioni mbili na nusu
Siku hizi mabasi yanabeba sana vifurushi na mizigo na vinaingiza hela nyingi sana
Jumla safari moja inaweza kupatikana milioni tatu
Mafuta=milioni
Wafanyakazi na mengineyo=milioni
Boss=milioni
Mara miaka miwili boss ananunua chuma mpya
Anakuwa nazo mbili
 
Scania kwa 710 Mil = wachina wawili, na kama wakiacha kuweka vile vitaa vya rangirangi nyingi wanavyochanganyikiwa navyo waluguru, basi ni wachina watatu
 
Kodi za bus kama sijakosea n milion 3, flat rate
 
Pikipiki inanunuliwa Kwa Milioni 3, na inapakia abiria 1 tena Kwa buku na baada ya miezi 18 inarudisha faida Kwa mmiliki na dereva wote wanapata faida.. Fikilia zaidi
 
Unadhani why lilihama kutoka kwa Sauli na kwenda kwa Katarama Hilo basi
 
hio 2.5 jumlisha na fungu lingine la mizigo kama kama kamilioni plus hivi kamejificha humo
 
Mkuu,
Kwa mawazo yako huwezi kuwekeza maana hata sisi binadamu mwisho wetu Ni kifo

Wekeza Kama kesho haipo
 
Ili upige hesabu sahihi za biashara unahitaji kujua umbali wa kutoka point A-to-B

Bei ya bus

Durability (longevity) lina uwezo wa kwenda miles ngapi kuanzia jipya (au uliponunua), hadi kuwa mkangafu (ili uweke na hela ya kununua lingine).

Siku ngapi kwa mwaka litakuwa barabarani

Idadi ya viti kwenye bus

Uwezo wa bus kula mafuta ya litre moja per mile, bei ya mafuta kwa litre.

Unafanya full services kila baada ya miles ngapi na gharama zake.

Matairi yana uwezo wa kwenda miles ngapi kabla ya kutakiwa kubadilishwa.

Bei ya tairi moja

Asilimia ngapi ya administration costs za ofisini unataka basi libebe

Fees za serikali kwa mwaka

Insurance cover kwa mwaka

Mshahara wa madereva, konda na mhududumu kwa mwaka.

☝️Hizo info unaweza fanyia hesabu za cost ya kuendesha basi kwa mile 1, wewe sasa uamue kiasi gani cha faida uongeze kila miłe moja kwa kiti.
 
Kuna pesa inapatikana kwenye mizigo pia.
 
Ungeiwekea namba huu ufafanuzi nadhani ndiyo jibu sahihi la thread hii..
 
Ungeiwekea namba huu ufafanuzi nadhani ndiyo jibu sahihi la thread hii..
Binafsi sina biashara ya bus

Sijui bei ya bus

Kila bus manufacturer anashauri wake ufanye full services baada ya miles elfu kadhaa

Sijui umbali wa Dar-Kahama

Administration costs za ofisi

Mfanyabiashara ana ma-bus mangapi ili hizo administration azigawe kwa mabasi

Sijui kutoka Kahama mpaka Dar bus lina madereva wangapi, mshahara wao ni kwa trip au kwa mwezi

Ulaji wa mafuta la bus husika, etc na info zingine nilizoweka hapo kama insurance, license fees na tozo zingine.

Hizo ni info unazohitaji kufanyia services costing ya bus upate unit cost per mile kwenye biashara ya usafirishaji wewe sasa uamue uongeze faida kiasi gani.

Weka details nikupigie hesabu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…