Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Wanabodi,
Hii ni makala ya Kwa Maslahi ya Taifa, kwenye Nipashe ya leo
Utambulisho
Japo mnanitambua kama mwana jf mwenzenu, kwenye mada very serious kama ubatili wa Katiba na ubatili wa sheria, naomba kujitambulisha tena na tena kuwa mimi sio tuu ni member wa jf ambaye ni mwandishi wa habari na mtangazaji wa kujitegemea kwa kujitolea, mimi pia ni mwanasheria na Wakili wa kujitegemea pia kwa kujitolea, ila uwakili wangu, nimeamua kujikita katika utoaji wa elimu kwa umma ya katiba, sheria na haki
View: https://youtu.be/ZJIKhnZCf04?si=BlJB95S62juYBqum
Hivyo mimi sio wakili msomi wa kwenda mahakamani, mimi ni wakili mtangazaji muelimishaji umma.
Kama kawa, kila nipatapo fursa, huja na makala elimishi za kwa maslahi ya taifa, ambazo huwa na maswali yakifuatiwa na hoja, kisha majibu utayaweka mwenyewe, swali la leo ni kuhusu badhi ya wasaidizi wa Rais Samia kama wanamsaidia au wananuogopa hivyo they are just good for nothing?.
Swali lenyewe ni hili.
"Wasaidizi wa JPM walimuogopa hadi kushindwa kumsaidia, Je wasaidizi wa Rais Samia wanamsaidia kwa kumweleza ukweli au nao pia wanamuogopa?. Vipi sisi wananchi wa kawaida tukiwemo sisi wana jf, tumsaidie au...?"
Naomba kutolea mfano wasaidizi wa JPM, walikuwa wanamuogopa sana hadi kushindwa kumsaidia!.
Marais wetu sio wanasheria, hivyo kwenye hoja za kikatiba, kisheria, kiutaratibu na kikanuni, wanawategemea wanasheria kuwaongoza kwa kumwambia ukweli. Wasaidizi wa JPM walimuogopa,
matokeo yake, walimuacha hadi aliikanyaga Katiba katika baadhi ya maamuzi yake, ikiwemo kupiga marufuku mikutano ya Siasa. Kwa vile Rais sio mwanasheria, anapofanya jambo lolote kinyume cha Katiba na kinyume cha sheria, ni wajibu wa wasaidizi wake sheria kumweleza kuwa hili ni kinyume cha Katiba na kinyume cha sheria.
Wakati JPM akipiga marufuku mikutano ya Siasa, alifanya hivyo kwa nia njema, bila yeye kujua ni kinyume na katiba, wasaidizi wake sheria walipaswa kumsaidia. Sisi huku mitaani kwanza tuliamini ana washauri wazuri na wanamsaidia Naamini Rais Magufuli ana washauri wazuri na anashauriwa vizuri tuu! , Ila... kisha tuka note baadhi ya mambo ni ndivyo sivyo, hivyo tukawashauri Wasaidizi wa Rais, Please Msaidieni Rais Wetu Kwenye Public . Msimuachie Kila Kitu Peke Yake! . tukamshauri AG, AG, Mshauri Mh.Rais Atoe Maagizo kwa Presidential Decrees Kuyapa Nguvu ya Kisheria
Siku ile pale Ikulu, nilipouliza swali hili
View: https://youtu.be/Ta0URHvUlko?si=NM2_ru-wuMLXu5oN
Ilitarajiwa wasaidizi wake sheria kujitokeza na kusaidia kumjibia boss wao, lakini walijikausha as if hajaulizwa kitu, na kitu alichojibu ndilo jibu la swali aliloulizwa!, sio kila anachofanya Rais ni kitu sahihi, wasaidizi wapo wanapaswa kumsaidia Rais wetu to do the right thing and do it right!.
Hili la kupiga marufuku mikutano ya Siasa limeendelea hadi alipoingia Rais Samia, akalirekebisha, kwanza tulimshukuru Rais Samia Asante Rais kuruhusu mikutano, tunakuomba uruhusu haki nyingine ambayo imeporwa ya Watanzania wote kuchagua na kuchaguliwa ila hatukuishia kushukuru tuu, bali pia tulitoa angalizo Anayekuja pasi na hodi, huondoka pasi kuaga. Kuzuiwa bila kifungu, kuruhusu bila Kifungu. Ni hisani ya Rais Samia. Haki kuhisaniwa hadi lini?
Je sasa, wasaidizi wa Rais Samia, nao pia pia wanamuogopa kama wasaidizi wa JPM hadi kushindwa kumsaidia?.
Rais Samia mara baada ya kuingia madarakani, alianza vizuri kwa kuondoa makando kando ya mtangulizi wake, hivyo kutupa matumaini makubwa, kuwa everything is going to change for the better.
Mimi ni miongoni mwa waandishi tulioandika makala mfululizo kumshauri hili na lile, na baadhi ya makala hizo ni hizi
Baada ya Rais Samia kuunda kikosi kazi, sio tuu tulimpongeza sana, bali pia tulitoa maangalizo
Tunajiuliza hivi hawa wasaidizi wa rais sheria wanamsaidia Rais wetu?.
Mfano "Jee Rais Samia anajua kuwa Katiba yetu ina ubatili fulani, uliochomekewa kiubatili hivyo kuifanya Tanzania kuwa na katiba Batili?. Je anajua kuwa hii sheria mpya ya uchaguzi aliyosaini hivi karibuni ni sheria batili inayokwenda kinyume cha Katiba ya JMT ya Mwaka 1977?. Jee anajua ubatili huu unadhulumu haki ya Mtanzania kuchagua na kuchaguliwa?. Jee anajua kila dhulma ya haki, huwa ina consequences?.
Hili shurti la wanasiasa kudhaminiwa na chama cha siasa, ili kugombea uongozi ni shurti batili liko kinyume na katiba ya JMT ya mwaka 1977, na limechomekewa kiubatili ndani ya katiba yetu.
Kufuatia ubatili huu, unamaanisha katiba yetu ina ubatili, na sheria mpya ya uchaguzi ni sheria batili, Serikali imetunga muswada batili, Bunge letu likatunga Sheria Batili, na Rais akaisaini hiyo Sheria batili kuanza kutumika, kwanini serikali yetu itunge muswada wa sheria batili?, kwanini Bunge letu tukufu litunge sheria batili?, kwa nini rais wetu asainishwe sheria batili wakati wasaidizi wa rais sheria wapo?.
Swali ni Je Rais Rais Samia, anajua kuwa hii sheria mpya ya uchaguzi aliyoisaini juzi juzi, kwa jicho la kisheria ni sheria batili?.
Japo Rais wa Tanzania, ana kinga ya kikatiba ya kutokushitakiwa kwa makosa yoyote atakayotenda akiwa madarakani katika utekelezaji wa majukumu yake ya urais, ila ibara ya 56A imesema specific kuwa kinga hiyo ya rais kutokushitakiwa, inahusu makosa mengine yote, ila haihusu Rais anapovunja katiba ya JMT, anashitakiwa kwa mujibu wa ibara ya 56A.
The only excuse ya rais kusaini sheria batili kuanza kutumika, ni kwa vile Rais wetu sio mwanasheria, hivyo hategemewi kuujua ubatili wa Katiba, ila kwa vile anawasaidizi wake sheria, wakiongozwa na Waziri wa sheria na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, hawa ni manguli wa sheria, wabobezi na wabobevu ambao wanaujua kabisa ubatili wa sheria hiyo, na ubatili wa Katiba, lakini hawajamweleza Rais Samia kuhusu ubatili huu kwa excuse kuwa ubatili huu umefanywa na awamu zilizotangulia, Rais Samia kaingia kaukuta, hivyo wakamtungia tuu sheria batili kwasababu sheria ikiyokuwepo nayo ni batili lakini ilikuwa inatumika!.
Kuna kanuni ya the doctrine of separation of powers between mihimili inayokwenda na kitu kinachoitwa checks and balance inayoitaka kila mhimili kuwa kiranja wa mhimili mwenzake usikiuke mamlaka yake wala usikiuke katiba.
Ibara ya 64 (5) ya Katiba imetamka wazi kuwa katiba ndio sheria mama, sheria nyingine yoyote itakayo kinzana na katiba, sheria hiyo itakuwa ni batili. Anayebatilisha sheria batili sio Mahakama, ni katiba yenyewe, jukumu la Mahakama ni kuithibisha tuu huo ubatili na kutangaza kuwa ni batili, tangu siku Mahakama Kuu ya Tanzania ilipouthitisha ubatili huu na kuutangaza, kuanzia hapo ubatili huo unakuwa umeisha batilishika hapo hapo kuanzia saa hiyo.
Licha ya Mahakama Kuu ya Tanzania kuutangaza ubatili huu na kuubatilisha, lakini Serikali ya awamu ya Sita, bado imetunga muswada wa sheria wenye ubatili ule ule, na Bunge letu, likaupokea muswada huo batili na kuutungia sheria hali iliyowafanya wabunge wetu makini kugeuka kama sio makini, checks and balance inatoka wapi?!.
Bunge letu chini mwalimu wangu wa sheria pale UDSM, mwanasheria mbobezi na mbobevu, Dr. Tulia Akson, alipaswa kulitumia Bunge kuicheki Serikali kuwa haiwezi kututungia muswada batili, na Bunge lina mamlaka ya kuuondoa ubatili huo na kutunga sheria safi isiyo na ubatili, lakini Bunge letu, likatunga Sheria Batili na kumpelekea Rais Samia kuisaini!, jee Rais Samia anajua kuwa amesainishwa sheria batili?.
Kwavile Rais Samia anawaamini sana wasaidizi wake, wamemtungia muswada batili na Bunge likitunga Sheria batili, Rais Samia yeye amesaini with very clear conscious kuwa anasaini sheria halali bila wasaidizi wake kumweleza ukweli kuwa sheria hiyo ni batili, hivyo kwenye hili la ubatili wa sheria mpya ya uchaguzi, Rais Samia hana kosa kabisa, wenye makosa ni Serikali kutunga muswada batili na Bunge kutunga sheria batili!.
Swali la kujiuliza ni baada ya kelele zote hizi kuhusu ubatili wa Katiba yetu na ubatili wa sheria zetu, jee Rais Samia amezisikia?.
Naona maandalizi ya uchaguzi wa serikali za mitaa kwa sheria batili yanaendelea, na mwakani tunakwenda kwenye uchaguzi mkuu na katiba batili na sheria batili!.
Kwa vile Mungu ni haki, no one knows for sure kwanini yule aliitwa na kuondoshwa mapema, usikute na hii dhulma ya haki za Watanzania, zimechangia, naendelea kumsisitiza Mama yetu, if there is anything she can do to help out the situation Watanzania kurejeshewa haki zao, Mama Please do!, utabarikiwa, tutabarikiwa na Tanzania itabarikiwa!.
Naamini kabisa kuna siku iso jina, kilio hiki cha haki kitasikika!.
Nawahi kanisani misa ya pili, nikitoka, naongeza nyama na kuifupisha hii mada ili wale wa miteremko wateremke na wale wapanda milima wapande.
Mungu Mbariki Rais Samia, jicho ona lake liione hii dhulma kubwa ya haki ya Mtanzania kuchagua na kuchaguliwa airejeshe.
Mungu Ibariki Tanzania
Jumapili Njema
Paskali

- Samia ni mpango wa Mungu kwa Tanzania: Kwa hili atabarikiwa, Taifa litabarikiwa. Asante Mungu kwa Samia, Mungu mbariki Samia, Mungu ibariki Tanzania!
- Asante Mungu kwa Rais Samia: Ni Msema Kweli na Mtenda Kweli, Ni Msema Haki na Mtenda Haki. Je, Ataruhusu Ubatili Huu Kuendelea Ndani ya Katiba Yetu?
- Haki Huinua Taifa! Rais Samia kwa Kauli na Matendo ameonesha ni mtu wa Haki. Akitekeleza hili kama alivyosema, atabarikiwa, Tanzania itabarikiwa
- Rais Samia ana nia njema Watanzania wapate haki, ila Watanzania hawajui Haki! Je, Tumsaidie kuelimisha umma Katiba, Sheria na Haki au?
- Asante Rais Samia kwa kuwasisitiza watendaji wa vyombo vya haki kuwa haki sio hisani, bali ni stahiki. Watende haki, tubadili Katiba kurudisha haki
Baada ya Rais Samia kuunda kikosi kazi, sio tuu tulimpongeza sana, bali pia tulitoa maangalizo
- Pongezi Rais Samia, Serikali, Kukubali Kubadili Sheria ya Uchaguzi, Tume Huru ya Uchaguzi!. Tuanze na Katiba Kwanza Ndipo Sheria Au?.
- Madudu ya ajabu ya ubatili wa Katiba yetu, mabadiliko "fake" ya sheria na Tume ya Uchaguzi. Rais Samia asilaumiwe kwasababu yeye sio mwanasheria!
- Ombi kwa Rais Samia: Japo wengi wape, wachache pia wasikilizwe, Hoja ya kufanya minimum reforms za Katiba ni hoja ya msingi sana kuliko hata Sheria!.
- Mabadiliko ya Sheria Bila Mabadiliko ya Katiba,Sawa na Kula Bila Kunawa!. Je Watanzania Tuna Haraka Sana na Uchaguzi Hadi Tukimbilie Kula Bila Kunawa?