MAHANJU
JF-Expert Member
- Aug 26, 2014
- 5,252
- 8,003
Inasemekana baada ya chama CUF kutangaza kuwachukulia hatua kali za kisheria wajumbe wote walioleta vurugu tarehe 21.08.2016 katika mkutano wao, hatua hizo ikiwa ni pamoja na kuwafukuza uanachama baadhi yao na wengine kupewa onyo kali.Sasa ni bayana kua kundi hilo limeshagawanyika huku wengine wakidai kutumiwa na watu ambao wamepewa pesa kukivuruga chama hicho.
Jana nilipata kumsikia mjumbe mmoja kutoka bara ambaye pia alikua ni kiongozi mwandamizi ndani ya chama hicho akidai kwamba anashangaa kuona kwamba amebaki peke yake huku baadhi ya wajumbe wakirudi nyuma ilihali walikubaliana kwa kauli moja kwamba ni lazima Prof Lipumba arudi kwenye nafasi yake ile kwa namna yeyote ile kwa maana kama kuasisi chama hicho naye ana mchango mkubwa sana.Akiongeza kwamba hashangazwi na tabia ya kubadilika badilika kwani ndiyo hulka ya binadamu, lakini yeye bado ataendelea kukipignia CUF hata akivuliwa uanachama kwani kuna hata Ofisi ya msajili ambaye ndiye mlezi wa vyama vyote.
Aidha wajumbe hao wanaodai kua wameingizwa mkenge na kujikuta kuijiingiza kwenye msafara wasioujua wamesema hawako tayari kupoteza uanachama wao kwa sababu ya wachumia tumbo wachache wanaotumiwa kwa makusudi ya wapinzani wa CUF.Kwa kauli moja wamesikika wakisema kua wakati wa kikao kijacho wataomuomba radhi mwenyekiti wa kikao kilichopita pamoja na viongozi wakuu wa chama hicho.
My take,
Nami nafikiri kama kweli CUF wamedhamiria kuwaadhibu vikali vinara wachafuzi wa chama hicho na wafanye hivyo bila kumwonea mtu haya, Ushahidi wa kukivuruga chama hicho ulionekana bayana siku ya tar 21.08.2016. Wale wanaojirudi wapewe tu onyo kali na ikiwezekana waitwe mbele ya kamati kuu wajieleze ni kwanini wasichukuliwe hatua za kinidhamu?