Wasambazaji wa biashara za jumla hebu fanyeni haya kuwanusuru wanaolipa kodi TRA.

sliding

Member
Joined
Mar 3, 2017
Posts
82
Reaction score
57
Hebu tusaidieni watu wa TRA na ofisi za afya kuwadhibiti wafanya biashara wasio walipa kodi.Utakuta mathalani nimefungua biashara yangu let say ya ka baa.Na nimeamua kuwa mlipa kodi japo makadirio tunayofanyiwa sio rafiki.Lakini pembeni yangu kuna ka baa ka pombe za kienyeji hakilipi kodi kinalipia halmashauri na vile vile kinauza bia.Kwa kuwa maisha yamebana unakuta wanywaji wanakimbilia huko.Mimi ambaye ninatakiwa kulipa tra na leseni na wahudumu zaidi ya wanne siuzi.Hebu wahusika oneni hili.Na ikibidi kigezo cha kuuziwa bia za jumla au soda na vinginevyo uonyeshe TIN number ya biashara yako ndio uuziwe.Na msambazaji wa jumla aonyeshe nimemuuzia fulani mwenye TIN hii.Serikali nayo itengeneze kodi rafiki ambazo zitashawishi kila mfanya biashara kutokwepa.
 
Acha wivu wewe .

kama umekosa wateja usilaumu mtu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…