Wasanii 10 wa Bongo Flava waliowahi kubadili majina yao ya kisanii

mtengwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2011
Posts
1,602
Reaction score
864
Wasanii kumi wa bongo flava waliobadili a.k.a zao


Professor Jay

Mkongwe huyu alietokea kundi la Hard Blasters Crew (HBC), mwanzoni alikua anajiita Nigga Jay lakini baadae akaja na jina la Professor Jay.


Joh Makini

Wengi wameanza kumsikia baada ya kutoa ‘hao' ambapo alikua anatumia jina la Joh Makini, kabla ya hapo wakati anaanza mziki(hajatoka) alikua anajulikana kwa jina la Rapcha.


Shaa

Mdada ambae alitokea kundi la cocacola popstars la wakilisha ambapo alikua anajulikana kwa jina la Sarah, baada ya kuanza solo projects ndo akajiita shaa.

Mr Blue
Huyu jamaa alikua anajiita Lil Sama, baada ya kutoka na nyimbo ya blue ndipo watu wakaanza kumuita Mr Blue had leo jina la Lil Sama limesahaulika kabisa na anatamba na jina la Mr Blue.

Nyandu Tozi
Wakati yuko Dar Skendo na kaka mkubwa Dudu Baya alikua anatambulika kama Dogo Hamidu, baadae mwenyewe aliamua kuliua jina la dogo Hamidu na kujiita Nyandu Tozi.


Q Chillah

Enzi hizo anaanza game alikua anajulikana kwa jina la Q Chief, baadae akabadili a.k.a na kuanza kujiita Q Chillah.


Sugu

Kwa sasa ni mbunge wa Mbeya(M), lakini bado anatambulika kama msanii wa Bongo flava na mmoja kati ya wakongwe wa mziki huo. Alianza miaka ya mwanzoni mwa 1990 na jina la 2 Proud na baadae Mr Two hadi mwanzoni mwa miaka ya 2000 alipojiita Sugu.


Nikki wa Pili

Wengi walianza kumjua baada ya kushirikishwa na kaka yake Joh makini kwenye Niaje, Ni vipi. Kabla ya hapo alikua anajiita Nikki Makini lakini aliamua kubadili jina na kujiita Nikki wa Pili.

Ongezea...
 
Sog Doggy- Chief Rumanyika
Dudubaya-Duduzuri ingawa halikuhit
 
Joh Makini nakumbuka hilo jina la Rapture alikuwa analitumia kama a.k.a...
 
9. O Ten huyu jamaa alibadilisha jina baada ya kuhamia La Familia na kujiita Nyandindi.
 
Inspector Haroun - Babu
Y-Thang - Solo
Double G - Dudubaya
Sir Nature-Juma Nature
 
Y Thang alikuwa Kwanza Unit na sasa ni daktari, Solo Thang baada ya jamaa kwnda uk kusoma akaamua kutumia stylr yke dats y fid q akasema Y Thang ghafla akageuka Solo .
Kwa hyo sio a.k.a bali ni watu wawili tofauti
 
young komba kabla hajawa kapteni na kujiita kapteni john komba
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…