Wasanii 10 wa filam na Muziki wenye mafanikio Bongo

mathematics

JF-Expert Member
Joined
Feb 21, 2012
Posts
3,322
Reaction score
1,110
Jana kwenye clouds tv wametoa majina kumi ya wasanii wenye mafanikio Bongo kwenye muziki na filamu. Majina ni kama ifuatavyo.

1. Mzee Yusuf
2. Lady Jay dee
3. Kanumba
4. Ray
5. Rose mhando
6. Professa Jay
7. AY
8. Diamond
9. JB
10. Ali kiba

Kwa ukweli sijui wametumia vigezo gani haswa labda kama ni ukongwe/umaaraufu/pesa/heshima/mchango etc hawakubainisha wazi.
Kwa ku-assume vigezo vyote hivyo au kimojawapo kwa maoni yangu nahisi kuna wasanii waliostahili zaidi kuwepo top 10 lakini hawajawekwa, mfano Mr. II . Hakuna ubishi katika wasanii wote wa kizazi kipya huyu bwana kapata mafanikio kuliko wasanii wote, mchango wake kwa muziki wa kizazi kipya, kwa wingi wa albamu alizitoa na mafanikio zaidi alipoutwaa uheshimiwa, huyu alistahili kuwepo kwenye top 10! Wasanii wengine ambao nahisi nao walistahili kuwepo top 10 ni Monalisa, Juma Nature, Ray C, Khadija Kopa, Kapteni John Komba

Unaonaje wewe hiyo list ya clouds? Msanii gani hakustahili kabisa kuwepo top 10, na msanii gani alistahili zaidi kuwepo top 10? na wewe je unaweza kutupa top 10 yako ya wasanii 10 wenye mafanikio Bongo?
 
mie naona wako sawa tu,kumuweka Sugu kwenye iyo list ni kumdhalilisha....

Ila sijamuona MwanaFA au kwa kuwa kajitoa TFU na kuomba amani na Sugu...

We mtu kama Ali Kiba ana mafanikio gani ya kumzidi Ali Choki?au wanafikir wotei atuyajui maisha ya wasanii.
 
Jamani mm nafikiri, Kira mmoja aweke wazi yeye mwenyewe mafanikio yake, Kama wasanii wa ulaya.
Tujue Ana keshi kiasi gan? Na Ana Maliki nini? Kodi kwa mwaka analipa kiasi gan?
Wakiweka hivyo utapata takwimu kirahisi.
 

Ndio maana nikasema sijui wametumia vigezo gani, kama ni ukongwe Diamond ana miaka mitatu tu toka atoke na kuwa juu kwa sasa... Ali Kiba hawezi mgusa Ali Choki kwa ukongwe... Kweli hata Mzee Yusuf hana ukongwe wa miaka zaidi ya mitano toka atoke na kuwa juu kwa miaka mitatu nyuma hadi sasa...
 
Mafanikio ni dhana panasana na kila mtu au kundi la watu wanaweza kutafsiri mafanikio kulingana na vigezo na malengo aliyojiwekea. Mafanikio si lazima yawe katika kupata pesa tu, yanaweza kuwa kuwepo kwenye game kwa muda mrefu, kutoa album nyingi kwa muda mfupi, nyimbo zako kupendwa zaidi, mahusiano yako na kituo fulani cha redio au TV, kufanya show iliyokusanya wetu wengi zaidi, kutwaa tuzo nyingi za KTM n.k Kwa maana hiyo, hiyo list hapo juu inabaki kuwa si kweli kwa upande mmoja na ni kweli kwa upande mwingine hadi pale waliotoa hiyo list waweke wazi vigezo walivyotumia.

 
Hatujui wametumia vigezo gani so ni ngumu kusema nani anastahili au lah! BTW hivi AY mafanikio yake ni yepi?au mazoea tu?
 
Hivi lile Tangazo la la uzazi wa mpango ile nyumba ndo ya mzee Yusuph kweli wasanii wa bongo wana maendeleo
 
Hatujui wametumia vigezo gani so ni ngumu kusema nani anastahili au lah! BTW hivi AY mafanikio yake ni yepi?au mazoea tu?

hahaha, labda kupata show matamasha ya nchi za nje.... Europe/Uarabuni/South Africa/USA
 
ha ha ha namie nilikuwa najiuliza hvo hvo! au labda mafanikio yanahusisha na idadi ya wake ulionao?!!
 
Hivi lile Tangazo la la uzazi wa mpango ile nyumba ndo ya mzee Yusuph kweli wasanii wa bongo wana maendeleo
ndio kwake pale kwa mfalme mzee yusuf. Maendeleo kwa kupiga pamba . Hiyo list wangefutwa wote abaki lady jaydee tuu
 
Walisema amejenga nyumba kumi
na anamiliki duka la kifahari.

Nyumba kumi?? Hv clouds wanajua nyumba? Usikute ana pagale mabwepande au madale wao wanaita nyumba,kama yeye ana nyumba je kina maige wasemaje? Duka la kifahari? Lipo wapi mcity,quality centre,shopper plaza,haidery au may fair plaza? Kama duka lenyewe ndio lile la used tv na majagi ya umeme basi imbombo ngafu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…