wasanii acheni kutania Ramadhani.

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
5,497
Reaction score
4,775
1)Ndugu zangu nawaasa,haswa haswa wasanii

Natumia hu wasa,kusema nanyi jamii

Mfanyao mambo sasa,kutania kwa bidii

Kutania Ramadhani,tabia yota mizizi.



2)Video mwazitengeza,mkivifanya vituko

Ukweli nawaeleza,hilo kubwa sikitiko

Hakuna mnachowaza,hiyo Sanaa ukoko

Kutania Ramadhani,Tabia yota mizizi.



3)Nyinyi mnajidhania,mnatoa burudani

Hakika mnakosea,mnapotania dini

Ramadhani nawambia,siyo tungo za kubuni

Kutania Ramadhani,tabia yota mizizi.



4)Wengine wanamuziki,wameitungia nyimbo

Nahisi wasaka kiki,hilo kwao kubwa jambo

Na bado hawasikiki,mambo yanakwenda Kombo

Kutania Ramadhani,tabia yota mizizi.



5)Shekhe eti wamwigiza,ala mchana kweupe

Eti sa hajochunguza,anafuturu viepe

Ghafula ajishangaza,mchana tena peupe

Kutania Ramadhani,tabia yota mizizi.



6)Na sisi twajichekea,shahari akichezewa

Muda unajiendea,ka vile tujaelewa

Wao wataendelea,sa tumeshachelewa

Kutania Ramadhani,Tabia yota mizizi.


SHAIRI- KUTANIWA RAMADHANI

MTUNZI-Idd Ninga,Arusha.

+255624010160

iddyallyninga@gmail.com
 
Sasa mkuu mm nilikua nasema kuwa usanii in dini tosha hakuna haja ya wasanii kujinasibisha na dini flan
Mara ukristo mara uislam
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…