Wasanii bongo movie na ishu ya ubunge !!!

lazima ukae

JF-Expert Member
Joined
May 15, 2013
Posts
791
Reaction score
414
Heshima kwenu wakubwa kwa wadogo,

Tangu mbunge wa mbeya mjini muheshimiwa sugu alipoonyesha nia ya dhati ya kugombea ubunge kwa tiketi ya CHADEMA na kufanikiwa kupata kiti hicho mwaka 2010,kumekuwepo na wimbi la wasanii wa bongo movie ambao nao wameonyesha nia kugombea ubunge katika uchaguzi ujao.

Baadhi ya wasanii hao ni Jb,Dude na shilole ambae nae ameonyesha nia ya kugombea ubunge wa jimbo la igunga mwaka 2015.Kitu ambacho nimekua nikijiuliza ni kwamba je wasanii hawa na wengine ambao watajitokeza wana nia ya dhati ya kuwawakilisha wananchi bungeni ili kutatua shida zao kama maji,umeme,elimu na huduma za afya au wanataka tu kugombea ubunge kwaajiri ya maslahi yao binafsi ?

Nasema hivyo kwasababu tumeona wagombea wengi sana kipindi cha uchaguzi wakija majimboni kwetu kuomba kura na kuorodhesha vitu watakavyovifanya pindi watakapopewa ridhaa ya kutuwakilisha bungeni ambapo mara baada ya kupata ubunge hawaonekani tena majimboni mpaka uchaguzi unapokaribia ndipo wanapoleta sura zao huku wakiona aibu baada ya kushindwa kutekeleza mambo waliyohaidi kwa wananchi

Je wasanii wetu wa bongo movie wataweza kutatua kero za wananchi au nao ndo walewale ?

Karibuni wadau tuweze kubadirishana mawazo.
 
Ha ha ha ha Shilole,Haya jamani mpigieni kura apite...
\\


Nilisikia mwingine yupo kule kwenye mji wenye sifa zote kasoro maji mengi yenye chumvi na kuhimili meli kubwa kubwa
 
Shilole hawezi kupata ubunge yeye aendelee tu kukata mauno
 
Ni mwendawazimu pekee ambaye anaweza kuwapigia kura hao.
 
Ni mwendawazimu pekee ambaye anaweza kuwapigia kura hao.

Kama kuna watu walipigwa jua kwenye foleni ili kumpigia kura prof. Maji marefu basi wapo pia watao wapigia hao wasanii
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…