Wewe ni mtu mwenye roho mbayaMkuu, waache hao wapuuzi
Wangekua wanafanya show, wanapiga pesa hafu wanakaa kimya tungejua ni wachakarikaji.
Tatizo linaanza wanaanza maneno ya kejeri na dharau mitandaoni.
Yaani wamevuka mipaka. Kusema kweli kwa upande wangu kuwasamehe ngumu sana
View attachment 3514526
Nimefuta nyimbo zao za recently zote nimebakisha old bongo fleva ambao 99% hawaimbi tena.
Wacha tupoteze wote
Sasa kwa nini manalialia wakiomba msamaha? Unaombaje msamaha bila kufanya kosa?Serikali ya CCM haijawahi na haitawahi kumlazimisha msanii kuunga mkono itikadi zake. Huwa ni hiari yao wenyewe kuunga mkono itikadi ya CCM. WASANII WAKO HURU KUCHAGUA UPANDE WA KISIASA WANAOTAKA. NI HAKI YAO YA KIKATIBA.
King Kikii, Mpongo love, Monique seka, Tshala Muana, Mbilia Bel n.k wanamjua sana muziki.Fally Ipupa Nsimba anaimba vizuri sana, Ferre Gola répandre anaimba vizuri, nimechelewa sana kulijua jambo hili
Sawa waendelee kuwaimbia hao wahuni wa kijani,ila sisi wananchi tunao tekwa,kuuwawa na kubambikiwa kesi za hovyo hatuwataki.Wakuu kabla ya kuwahukumu hawa viumbe tujikumbushe kuwa wasanii ni watu wenye ushawishi mkubwa kwenye jamii kuliko hata wanasiasa walio wengi. Kwa mfano Diamond peke yake ana ushawishi mkubwa kuliko wanasiasa wote wa nchi hii... kidunia hakuna Rais, mfalme au mtawala yeyote aliyekuwa akimzidi ushawishi hayati Michael Jackson kipindi akiwa hai.
Tawala karibu zote zinajua hilo ndo maana huwa zinawaweka karibu wasanii kwa kuwashawishi au kuwalazimisha kwa sababu kwa ushawishi walio nao ni hatari kuwaacha tu. Wakihamia kambi pinzani ni hatari kubwa. Wasanii wengi wamewahi kujikuta matatizoni kwa kusimama na itikadi tofauti na serikali iliyoko madarakani.
Mfano mrahisi ni majirani DRC zamani wakiitwa Zaire chini ya Dikteta Mobutu. Wasanii walipitia magumu kila walipokuwa wakionyesha misimamo yao inayokinzana na serikali. Hayati Franco aliwahi kukimbia nchi. Koffi Olomide mwaka 97 kama sio 98 aliwahi simamishwa barabarani na kushushwa kisha kucharazwa viboko na askari kama mtoto mdogo. Werrason alishushwa jukwaani akiwa anatumbuiza na kushushiwa kipigo cha mbwa mwizi. Kimsingi ni hatari kwa msanii kuwa na itikadi tofauti na serikali iliyopo madarakani. Hapa Tanzania mifano ipo na mnaijua.
Ninawasihi watanzania wote tusamehe hawa vijana kwa sababu wasingeweza kuepuka kukinywea kikombe walichokinywea.
Wema,mlimpima mkojo kisa alikua chadema,acheni upuuzi.Serikali ya CCM haijawahi na haitawahi kumlazimisha msanii kuunga mkono itikadi zake. Huwa ni hiari yao wenyewe kuunga mkono itikadi ya CCM. WASANII WAKO HURU KUCHAGUA UPANDE WA KISIASA WANAOTAKA. NI HAKI YAO YA KIKATIBA.