Wasanii kushindwa kujigharamia matibabu nini tatizo?

Diamond ndio kaja kuwafungua na kuwatoa wasanii tongotongo...yenyewe yalikua yanajisikia ufahari tu kuonekana kwenye tv bila kupata hata sumni
 
Je na sis rai wa kawaida ni wangapi ambao tumejitahidi hata angalau kuwekeza katika maisha yetu? Maana isije tukawa tunajidai kuwananga wasanii wakati sis wenyewe kumbe ndo walewale, BIMA ya afya tu tukiambizana kukata inakuwa vita
ni kweli hata kwa watu wa kawaida kuna la kujifunza ila wasanii mara zote wakiumwa ni watu wa kuchangiwa hawajifunzi kwa wenzao hicho kidogo wanacchopata kukata bima ya afya nhif unaweza pata hata million moja kwa mwaka
 
ni kweli hata kwa watu wa kawaida kuna la kujifunza ila wasanii mara zote wakiumwa ni watu wa kuchangiwa hawajifunzi kwa wenzao hicho kidogo wanacchopata kukata bima ya afya nhif unaweza pata hata million moja kwa mwaka
Ni kweli mkuu ila wasanii hao hao ndo wametoka katika jamii zetu hizi kwa hiyo njia pekee kwa sasa ni kujifunza kutokana na makosa
 
Aliinvest sana kwenye vitoboziiiii

OvA
 
Gharama za matibabu haziwasumbui tu wasanii peke yao...

Hata watu wenye kazi zao na wanapokea mishahara kila mwisho wa mwezi, swala la matibabu ni mtihani sana...


Cc: mahondaw

uko sahihi sana

nina mifano ya mainjinia wengi wanaomba msaada ya kutibiwa india


nina mfano wa lecturer mmoja pia......


list goes on
 
Huyo mzee anapesa za kutosha tu kumwezesha na matibabu yake.
Anamiliki nyumba zaidi ya moja kwa nini asiuze akajitibu?
Mbona sisi tukiumwa tunatumia mali zetu kujitibu iweje wao wasanii watembeze bakuli mfano yule Wastara anaishi kwenye jumba kama lile alishindwa kujilipia matibabu kweli hadi Rais akampatia ile 16mil.?
Umefika muda sasa kuwakataa na shida zao, kazi wanafanya na pesa wanapata sema wanajichukulia kama watu wa jamii so hata matatizo yao wanaibebesha jamii nzima.

Kila mtu abebe msalaba wake.
 
Mimi nina maoni tofauti kidogo..Mimi nadhani gharama za kwenda kutibiwa india ni kubwa sana labda kufanya wasanii kushindwa kumudu sijui lakini?
Huko India imekuwa recommended na Dr kuwa aende au wameamua tu Kwa vile ni msanii?
 
Majuto kapiga hela nzuri tu.
Majuzi kapata tenda ya Neel salt
Au mzee anapenda chuchu saa sita ?
 
Tatizo ni usanii hadi kwenye maisha halisi. Mtu yupo Tabata kapanga vyumba viwili, lakini Insta anapost location za kushutia video yake
 
Nadhani wanakosa focus wenyewe kwa kushindwa kuinvest pesa wanayopata kwenye mambo makubwa ya maana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…