Wasanii Mlio kwenye kilele cha mafanikio jifunzeni kuweka akiba

usomdudu

Senior Member
Joined
Dec 18, 2011
Posts
114
Reaction score
102
Greetings wakuu!

Nimesikitishwa sana na kauli ya bwana ROMA MKATOLIKI kwamba ameshindwa kumpeleka mwanaye shule kwa kukosa karo kutokana na 'kufungiwa' kwa miezi 6 kutojihusisha na sanaa na BASATA

Inawezekana ameongea kutafuta 'public sympathy' na ndo maana akamchkua mtoto wake kwenda naye kwenye interview radio, kama ndivyo amefanya makosa sana (Bila kujali sababu za kufungiwa kwake)

Pointi ya msingi yeye pamoja na wasanii wenzie wanifunze kujiwekea akiba kwa maisha yao ya baadae, kulalamika kwamba umekosa karo ni Aibu sana kwa msanii kama yeye ambaye records zinaonyesha tangu 'ametoka' hajawahi kukaa kijiweni, Wasanii wetu wanahitaji msaada mkubwa sana kinawazo jinsi ya kukuza pato lao wanalopata liweze kuwa msaada baadaye.

Sote tu mashahidi wako wasanii wengi waliokuwepo kipindi cha nyuma na walipata pesa nyingi ila leo wako 'vijiweni' na wanahangaika sana kujaribu 'kutoka' tena lakini inashindikana matokeo yake wanaishia kwenye mihadarati sababu ya 'frustrations' na mwishowe huwa mbaya (mifano ipo).

Hii iwe kama 'woke up call' kwa wasanii wetu kwamba kidogo wanacho kipata leo kesho hakitakuwepo na wakitumie vizuri kuwekeza sio kufanyia starehe zisizo na faida yoyote!

Kiroho safi, Asante!
 
hlf kwa kuongezea kwmb Roma hizo show ni kwamba anapata kila siku? maana km kufungiwa ni kafungiwa juzi tu hapa...sasa cjui alikuwa bdo hajatenga ada ya mwanawe? maana hayo yangekuwa relevant sana km angekuja kuyaongea after 6 months ili kuonesha ni kiasi gani kitendo cha kufungiwa kimemuathiri kimaisha...lkn saa hivi ni mapema sana kusema kufungiwa kumemfanya akose ada ya mwanawe.
 
Kazunguka FIESTA mikoa yote,inamana walikuwa hawamlipi,hapo bado show zake binafsi na kundi la ROSTAM au izi show hawalipwi.Wangelalamika wasanii wengine ila si ROMA au labda anataka BASATA na Bi Shonza wamuhurumie.
 
Inawezekanaa Tuu labda hela alizopata Kipindi kilee kafanyia Mambo mengi.. Na roma ni msanii bado kuna hela kwa ajili ya Studio..mahitaji nyumbani...!! Show zenyewe wanalipwa sh ngapi jamani??????? Angekuwa Mond sawaa
 
TATIZO LA WASANII WANAPENDA KUISHI KISANII,KUPANGA JUMBA LA GHOROFA KODI LAKI 7,BATAZ SANA VIWANJA VIKALI ETC.
 
Nini ada wengine wanalalamika kukosa pesa za pampaz za watoto

Napita tu,mie sijataja mtu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…