Halafu kuna mijitu inasimama hadharani na kuwatetea wanahusika na kusambaza madawa eti oo wanaonewa. Sasa hawa tunawaona kwa vile walikuwa watu maarufu. Je kuna vijana wangapi wanaangamia na mihadarati. Sote tuungane kwa pamoja ktk vita hii. Tusifanye siasa maana madawa yanatuathiri wote bila kujali vyama vyetu. Makonda amethubutu ni zamu ya watanzania sasa kuthubutu. Tutoe ushirikiano pale tunapoona inastahili, kama njia inayotumika unahisi si sahihi toa maono yako na si kubeza jitihada za wengine.