Raymanu KE
JF-Expert Member
- Jan 20, 2022
- 8,611
- 16,118
Ken Walibora- Kidagaa kimemwozea
Hayati Ken Walibora- alikuwa mwandishi wa vitabu vya fasihi kutokea nchini Kenya.
Kwenye kitabu chake kimoja kinachoitwa Kidagaa kimemwozea alikuwemo mhusika mmoja aliyeitwa Mtemi Nasaba Bora.
Mtemi alikuwa kiongozi wa kimla na aliwatesa Sana watu wake.
Alikufa kifo Cha ajabu Sana kwani alipatikana na baadhi ya wanachi akiwa amekufa kifo tatanishi sana msituni afu gari yake imepakiwa kando ya huo msitu.
Mazishi Yake yalihudhuriwa na watu wachache Sana.
Mwako 2021 kipindi Cha Corona mwandishi Ken Walibora alistukiwa na watu kadhaa msituni akiwa amefariki na gari yake imepakiwa kando ya maiti yake.
Mazishi yake yaliandaliwa haraka Sana na kuhudhuriwa na watu wachache kwani kipindi hicho Corona ndio ilikuwa imepamba Moto kwahyo serikali ya Kenya iliweka vikwazo na sheria mbali mbali kuhusiana na mikusanyiko ya watu kwa lengo la kudhibiti kirusi Cha Corona.
Sam Wa Ukweli- Walimwengu
Walimwengu ndio ulikuwa wimbo wa mwisho wa msanii marehemu Sam Wa Ukweli.
Sam aliimba huo wimbo kwa hisia Kali Sana akielezea magumu aliyokuwa anapitia kipindi Cha uhai wake.
Verse ya kwanza aliimba Kama anatoa shukrani za mwisho kwa Mungu pamoja na watu wote waliomzunguka na aliimba kwa hisia Kali Sana Hadi akawa Kama analia hivi.
Watu wengi akiwemo producer wake waliamini kwamba Sam alikuwa anatabiria hatma/ kifo chake kupitia wimbo wa "Walimwengu"
Diamond Platinumz- Utanipenda?
Kwenye wimbo Diamond aliyaongelea Mambo mengi Sana na Moja Kati ya hayo Ni pale alipoimba "Utasikia tafarani eti Dimond kwa Zari amemwagwa"- hiki kipande Diamond alikuwa anatabiria jinsi atakavyoachwa na Zari na Kweli iliyokea exactly.
Diamond pia alizungumzia suala la kufulia kimziki,kipesa,kutorokwa na mashabiki, managers( Babu Tale) pamoja na Marafiki afu baadae atajitahidi na kurudi kwenye game.
Kuna uwezakano hili nalo likatokea( japo simwombei imtokee hivyo) pia,, who knows?
Rayvanny- Natafuta Kiki
Kwenye huu wimbo Kuna mahali Rayvanny aliimba eti " nitoke Wasafi niende kwa kiba".
Sote tunajua tayari Rayvanny ameshaanza kuonyesha dalili za kuondoka kwenye label ya Wasafi na bila Shaka anaweza akaungana na Ali Kiba( in terms boc Music collaboration) na wakaendeleza shughuli ya muziki
Hio mifano michache Ni ishara tosha kuonyesha jinsi wasanii wa Sanaa mbali mbali walivyo na uwezo wa kutabiri hatma zao kwenye kazi zao.
Atakayekuwa na mifano mingine Kama hii ya kwangu Basi asisite kutiririka.