Wasanii na wachekeshaji maarufu duniani

NostradamusEstrademe

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2017
Posts
3,402
Reaction score
4,532
1.ROWAN SEBASTIAN ATKINSON(MR BEAN)

Alizaliwa 6th Jan 1955 Uingereza.Ni mchekeshaji, mtayarishaji wa filamu,na muandaaji wa vipindi vya filamu.Mtindo wake ni kuchekesha akijifanya kama taahira

ELIMU YAKE:-
1.Masomo yake ya sayansi elimu ya juu alipata alama za juu(distinction)
2. Ana shahada ya kwanza Bsc ya electrical and electronic engineering kutoka chuo kikuu cha Newcastle
3.Ana shahada ya uzamili Msc kwenye electrical engineering toka chuo cha Queen Oxford
4.Alitaka aendelee kusoma shahada ya uzamivu PhD lakini akagundua ana kipaji cha usanii uchekeshaji akaamua kujikita huko hadi sasa.

March 2001 alikuwa na safari ya likizo Kenya akiwa angani kwenye ndege yake binafsi jet rubani wake alizimia ghafla angani yeye mwenyewe akaingia kwenye usukani baada ya muda rubani akazinduka wakatua salama uwanja wa Wilson Nairobi.

Ameshawahi pewa tuzo maalum ya malkia.

2.SIR CHARLES SPENCER CHAPLIN (CHARLIE CHAMPLIN)
Alizaliwa 16th April 1889 Walworth London alifariki 1977.
Alikuwa mchekeshaji wa filamu za kimya kimya.Sifa zake zilivuma dunia nzima.

Kuanzia mwaka 1918 alianza kujulikana duniani.Taaluma yake ya kuchekesha ilidumu kwa zaidi ya miaka 75.

TUZO ZAKE:-
1.British empire
2.Doctor of letters shahada ya heshima aliyotunukiwa na chuo cha Oxford na Durham mwaka 1962
3.French government award
4.Hollwood award

Na zingine nyingi bila kutaja.

Nimeona nielezee kwa undani hao wawili ngoja niendelee kutaja watu wengine wasanii maarufu.

3.VOLODYMYR ZELENSKIY
Huyu ni ana miaka 41 ni mchekeshaji raia wa Ukraine amegombea Urais na mpaka sasa anaongoza kura za maoni hadi sasa.

4.RONALD REAGAN
Huyu alikuwa Rais wa Marekani na alikuwa mcheza sinema.

5.ANDRY RAJOELNA
Alikuwa anajulikana kama Disco jockey au DJ.Alikuwa DJ kwenye miziki alikuwa Rais wa Madagascar miaka 11 iliyopita na kwa sasa ndio Rais wa huko kwa mara ingine

Tuje nchini kwetu tujaribu kugusia baadhi ya wasanii wetu.Maudhui makubwa ya uzi wangu ni kuonyesha kuwa usanii ni kazi iliyotukuka ambapo humo humo vinaweza kutokea vipaji vingine kikubwa zaidi ni kuwa usanii ni ubunifu na kila msanii ana mtindo wake anaotumia kujitofautisha na wasanii wengine.Huo ni ushindani.

6.DR REMMY ONGARA
Huyu alipiga mziki wake akijiita Dr na kusema yeye ana sura mbaya.Wakati mwingine alikuwa alipanda jukwaani anapanda amevaa kibuyu na mahirizi.Alipatwa kuulizwa akasema yeye sio muumini wa ushirikina ila anafanya vile kama utambulisho wake wa uafrika na kujitofautisha na wasanii wengine.

7.JOHN WALKER
Alikuwa anaimba muziki wa mahadhi kama amelewa sana.KiukweliNa huyu jamaa alikuwa hanywi pombe ujumbe unafika kwa hadhira iliyokusudiwa

8.MR EBO
Aliimba katika mahadhi ya kimasai na mziki wake ulipendwa mno.

Usani ni fani kama fani zingine mtu hawezi mchagulia mtu au kumdharau mtu kuwa anaigiza isivyotakiwa kikubwa msanii asivunje maadili yetu na kuvunja sheria za nchi

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Piere liquid :huyu jamaa ni hatar fayaaa
Anavituko amazing analewa, Hana bifu na mtu
Mtu wa watu anapenda wengine wafugaji
Hana shobo na kiumbe chochote
Wanamtukana ila yeye kimya
Hapendi sifaaa
Ameitwa Kenya kiroho Safi
Kesho kutwa anaenda marekani halafu London uingereza
Yeye anapiga pesa tuu
Amekuwa ambassador wa biashara nyingi
Wajukuu wa Ibilisi na watoto wa shetan wanamuonea wivu
Ikiwauma kunywa sumu blalifuu zenu Sio lazima muishi kwenye hii dunia
Tuacheni tule raha zetu sisi
official piere piga Kazi
Tupe rahaaa mzee baba

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tupo tofauti sana..mimi nachekeshwa na hawa wajombaa

1. Adam Sadler
2. Jonah hill
3. Ben Stiller
4. Seth rogen
5.steve carrel
6. Jim Carey
7. Edie Murphy
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…