Wasanii wa Alikiba wasainiwa na Harmonize

crankshaft

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2019
Posts
1,427
Reaction score
3,438
Wasanii wawili waliokimbia label ya king's music ya Alikiba, Cheed na Killy hatimaye wametambulishwa rasmi katika label ya Kondegang ya Harmonize.

Kwa sasa label hiyo ina jumla ya wasanii 5 tangu kuanzishwa kwake ikiwa ni chini ya mwaka mmoja tu pia inasimamia kazi za msanii skales kutoka nchini Nigeria katika Afrika Mashariki.

Awali msanii Q Chila aliwahi kuhusishwa na label hiyo lakini karibuni alifunguka na kusema hakusaini Kondegang kwa sababu Harmonize hawezi kumlipa.

 
Asksr,
Huyu Harmonize naona hajui pa kushika ni wapi, alianza na Qchief hamukmfikisha kokote (Qchilla naye anageuza maneno kuna siku anahojiwa na Babu wa kitaa alisema kuna watu walimfitinisha Harmonize akasepa pasipo hata kumwambia sababu leo anasema hakuwa na uwezo wa kumlipa), akaja na Ibra naye sioni anakoelekea, mara kamsaini yule Mnaija naye hajafika kokote, sasa kawasign hawa madogo. Personally hawa madogo naona hata vipaji hawana walikuwa wanatembelea nyota ya Alikiba tu.

Ila muda utasema maana yeye mwenyewe Konde Boy naona siku baada ya siku kimziki anazidi kushuka, Konde wa sasa si kama konde wa kipindi yuko WCB baada ya miaka miwili sijui atakuwa wapi Mr. Konde.
 
Ibrah hujui anapoelekea unataka aelekee wapi labda ?
kwahiyo unampangia MTU mipango yake?
Kuwa amsaini nani si ndio?
Halafu skales hajafika popote hivi unamjua vizuri ama?
Skales ni msanii mkubwa tayari mpka huku tulimfahamu kabla ya hata kusign na konde gang.
MTU kama wewe hujawahi hata kuwepo hujawahi hata kuwepo kwenye industry ya mziki halafu unajifanya bingwa wa kutabiri maanguko ya watu
Harmonize akipotea wewe unafaidika nini?
 
Mafanikio ya kimziki hayajifichi, mtu akifanya poa anaonekana wazi kafanya poa. Time will tell....
 
Mafanikio ya kimziki hayajifichi, mtu akifanya poa anaonekana wazi kafanya poa. Time will tell....
Sasa hata mwaka haijamaliza unataka mafanikio ya namna gani.
Kila kitu kilianza chini hata wcb walianza na msanii mmoja huyo huyo harmonize Leo umeona walipo?
Huwezi kufika kumi usipoanza na moja
 
Sasa hata mwaka haijamaliza unataka mafanikio ya namna gani.
Kila kitu kilianza chini hata wcb walianza na msanii mmoja huyo huyo harmonize Leo umeona walipo?
Huwezi kufika kumi usipoanza na moja
Utaona mfano Zuchu anafanya poa, huwezi mcompare na Ibra achilia mbali kumlinganisha na Zuchu Ibra hafanyi poa huwezi kucompare hata kipinfi wakina Mario wanatoka.
Any way ngoja tujipe muda.
 
Utaona mfano Zuchu anafanya poa, huwezi mcompare na Ibra achilia mbali kumlinganisha na Zuchu Ibra hafanyi poa huwezi kucompare hata kipinfi wakina Mario wanatoka.
Any way ngoja tujipe muda.
Hivi wewe namna gani?
Unapokuwa wcb automatic unakuwa msanii popular. Wana die hard fans wao siku ukiondoka unawaacha pale mfano ni mavoko na harmonize.kama kweli ngoja uone zuchu akitoka wcb kama atapata mashabiki kama hawa wa wcb.
Ukiwa lebel kubwa unapata promo ,hutolei jasho ,mauzo ya kazi zako wanasimamia sasa huoni tofauti ilipo?
Kondegang ni ka lebel kadogo kanachoanza kujitutumua
Nilidhani upo makin kumbe
 
Ibra hafanyi vizuri in fact trend yake inashuka hata kuliko alipotoka... Konde mwenyewe ngoja tusubiri baada ya mwaka mmoja mbele tuone.
 
Ibra hafanyi vizuri in fact trend yake inashuka hata kuliko alipotoka... Konde mwenyewe ngoja tusubiri baada ya mwaka mmoja mbele tuone.
Haya bwana mtabiri ibrah mwanzo alikuwa wapi lebel gani akae kwa trend katoa wimbo?
Haya tabiri niambie tundu lissu atashinda urais?
 
Acha uongo mzee harmonize anafanya vizur Sana nyimbo zake labda Kama una chuki naye tu
 
Acha uongo mzee harmonize anafanya vizur Sana nyimbo zake labda Kama una chuki naye tu
Hana hit song kama kipindi kile, ilikuwa ni hit baada ya hit. Sasa hivi kawaida tu bado ana jina la moto na mbwembwe sijui zitamfanya akae kwa muda gani kwenye trend.
 
Bila shaka hii comment imeandikwa na kijana aliyemaliza chuo halafu jobless ambae hajui hata siku yake ataimaliza vipi, mara nyingi mnakuaga so bitter kwa vijana wenzenu waliotusua kimaisha halafu hawajasoma,

#No hard feelings tho#
#Panic at your risk#
[emoji38][emoji38]
 
Ba
 
Unapanic this is not personal ni mtazamo wa mashabiki wa mziki huna haja ya kupanic, kunywa glass moja ya maji chill up kidogo usije pata presha wa vitu vidogo.
Hakunaga maoni ya shabiki maandazi kama wewe
Haya ni maoni au makasiriko ?
Hahahhahh tafuta LA kufanya mkuu hili LA kukandia watu halikufai
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…