kuanzia miaka ya 2010 bongo muvi imezidi kupoteza mvuto kwa kasi ya ajabu...hii ni kutokana na ubora mbovu wa kazi zao...lakini kwa kipindi chote hiki media mbalimbali zimekuwa zikiwabeba mno...ukisoma gazeti utakuta "malkia wa bongo muvi wema sepetu, staa wa filamu tanzania yusufu mlela, mkali wa muvi za action tanzania j plus" kwa muvi gani wanazozitengeneza? ni hizi za kupiga risasi kwenye kioo, kioo hakivunjiki na mtu ndani ya gari anakufa kwa risasi hiyo, ni hizi unazoangalia unaona kivuli cha camera man, ni hizi ambazo part one na part two havina uhusiano...au zipo nyingine nzuri nzuri wameanza kuzitengeneza...labda me niko huku chibelela, zinachelewa kufika.....embu niambieni hawa watu wanatengeneza filamu gani hadi waitwe mastaa....