Wasanii wa bongo muvie wanastahili sifa wanazopewa na media?

Socw

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2016
Posts
1,329
Reaction score
2,644
kuanzia miaka ya 2010 bongo muvi imezidi kupoteza mvuto kwa kasi ya ajabu...hii ni kutokana na ubora mbovu wa kazi zao...lakini kwa kipindi chote hiki media mbalimbali zimekuwa zikiwabeba mno...ukisoma gazeti utakuta "malkia wa bongo muvi wema sepetu, staa wa filamu tanzania yusufu mlela, mkali wa muvi za action tanzania j plus" kwa muvi gani wanazozitengeneza? ni hizi za kupiga risasi kwenye kioo, kioo hakivunjiki na mtu ndani ya gari anakufa kwa risasi hiyo, ni hizi unazoangalia unaona kivuli cha camera man, ni hizi ambazo part one na part two havina uhusiano...au zipo nyingine nzuri nzuri wameanza kuzitengeneza...labda me niko huku chibelela, zinachelewa kufika.....embu niambieni hawa watu wanatengeneza filamu gani hadi waitwe mastaa....
 
Pamoja na ukweli kuwa viwango vya wasanii wetu viko chini,lakini media na tabia za watanzania kuchukulia vitu simple inachangia kwa kiasi kikubwa,ukisoma magazeti misifa isiyostahili wanayopewa wachezaji wa mpira,waigizaji,wanamuziki ukajumlisha na watanzania tunavyorahisisha vitu visivyorahishika kama elimu kwa kufungua vyuo vingi uchwara utagundua kwa nini vitu vyetu vinapoteza mvuto na thamani mapema sana.
 
Hakuna movie industry Tanzania and therefore hatuna Wasanii wa filamu hapa.
Take my word... Hatuna Wasanii wa filamu hapa Tz.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…