Wasanii wa bongo tuna ‘fake’ vitu vingi – Kassim Mganga

chinchilla coat

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2016
Posts
5,107
Reaction score
10,969
Msanii wa muziki, Kassim Mganga amesema wasanii wengi wa bongo wana ‘fake’ kuwa na maisha bora wakati hawapo hivyo



Muimbaji huyo ambaye ni mtunzi mzuri wa nyimbo za mahaba, amesema wasanii wengi ‘wanafake’ maisha yao ili walingane na mastaa wakubwa duniani.

“Mi ambacho nimejifunza, wenzetu hawa’act, wenzetu wako real, ndio maisha yako vile, ukimuona Chris Brown au ukimuona 50 Cent pamoja na umri wake aliokuwa nao leo, anaonesha magari yake na nini na nini, watu wapo kwenye ushindani wa biashara kubwa sana, kwa hiyo anachokifanya kina mantiki, sisi tumekuwa tuna’fake vitu vingi havipo real, lakini tunataka tuwaoneshe kwenye mitandao, tunadanganya, tunawadanganya sana mashabiki wetu, mashabiki wanatuona si watu ambao tuna maisha makubwa sana, wakati haiko hivyo kiuhalisia,” Kassim Mganga alikiambia kipindi cha Planet bongo cha EA Radio.

Pia muimbaji huyo amewataka wasanii wachanga kuacha kuiga maisha ya mastaa wa bongo ambao wanafake maisha yao ili kuwadanganya mashabiki wao.
 
50 Cent Testifies that his Lifestyle is Fake, Cars & Jewelry RENTED & He's Worth $4.4 Million!
 
Angesema kuwa yeye ndio ana "fake" asiwasemee wengine,la kama anachokisema kina ukweli basi awataje,kinyume na hapo ana zidi kuwa "fake"
 
Ni diamond pekee ambae naonaga hanaga haja ya kufake mana jamaa ana mipesa,,, kama wasanii hamna pesa acheni kuact ishini simple life kama za kina kingwendulile
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…