Wasanii wa Bongo wananunua wafuasi, njoo uone hili

nashukuru mzima

JF-Expert Member
Joined
Jul 11, 2017
Posts
1,014
Reaction score
1,903
Haujaelewa kitu boss ni kwamba nchi kama Nigeria watu wapo busy sana na mambo yao hawatumii sana mitandao ya kijamii japo wapo wengi kwa idadi kuliko tz, Tanzania social media ni big issue tofauti na nchi kibao kwa mfano UK uwa hawana matumizi makubwa ya social media ndo maana ata kufollow follow artists hawana muda ndo maan Kanye west na Jay Z hawaamini katika numbers maana uwa zinadanganya , ukilinganisha mafanikio ya wasanii na fan base zao kwa followers wa instagram unakuwa una fail,

Maana kwa mfano US wizkid ana fan base kubwa ambao hawatumii sana social media na hawana mpango wa kumfollow, nipende kusema tu wabongo bado washama wa insta😀😀na hao followers wengi wa wasanii wa Tanzania ni wabongo 😀😀watanzania hatuna shughuli za kufanya ndo maana ata tuzo za kupiga kupitia mitandaoni uwa watanzania wanashinda eti kuliko nigeria , wakati wanaija wapo wengi
 
Utashangaa Diamond insta ana 15M followers ila Twita ana 1M kama Maria Sarungi 🤣
 
Utashangaa Diamond insta ana 15M followers ila Twita ana 1M kama Maria Sarungi 🤣
Sasa Twitter si hawanaga habari na mtu ambaye hana habari nao, kila social media inasifa zake, Twitter uwa watu wanafollow watu ambao wana interact nao, hawapendi kumfollow mtu anayejikuta star sana na hachangii hoja au kujibu comments zao, ndo maana Twitter wasanii wanaokubalika bongo ni AY, JIDE, FA na FID ila hao wengine mtandao wao ni insta maana uko ndo wanashobokewa na kubabaikiwa, na kuna maboya wao
 
Umeongea point , lakini bado kuna ukweli kuwa wasanii wetu huwa wanaboost account , na hata comment , imagine mtu ana followers 2.5 milion alaf akipost , comment zinaishia 20 au 15, mwingine anapost ndani ya masaa 2 comment 1000 alaf zinaganda hapo hapo milele , ukichunguza comments unakuta kuna watu baadhi , mfano mtu mmoja tuu kacomment 20 times na caption ya 🔥... Basi tuu ionekane anafatiliwa , .... Siwezi kuhukumu Sana Ila watz janja janja nyingi ambazo zinatupa matokeo ya kijanja janja pia ...

Mimi Nina account moja ya biashara nimefungua Instagram , mpak sasa ina followers 600 tuu , na hao wamekuja baada ya kuvutiwa na bidhaa zangu ambazo mostly napromote , na mzigo unatembea , lakni cha kushangaza kila sku dm ni nyingi watu wananifata ooh naongeza followers , fanya accnt yako iwe na followers wengi , sasa unaniongezea followers ambao sio interested na bidhaa zangu utanipa faida gan ? Anyway ndo maisha yalivyo lakni
 
Kununua page ambayo hausiani na kitu unachoenda kuifanyia na kununua followers ni sawa na kujitekenya mwenye halafu unacheka😀😀
 
Sio kwamba wananunua. Jibu jepesi ni kuwa sisi wabongo bado ni washamba sana kwenye hii mitandao ya kijamii tofauti na wenzetu. Mtu yuko radhi asile ila anunue bando kisha aingie Instagram.
 
Ishu kubwa Bongo ni kuwa watu hawana ishu za kufanya na umbea ndio priority kwenye maisha yao.

Ila kwa bei za vifurushi zinavyotembea hayo yanaenda kuisha karibuni.
 
Bongo watu wengi wapo instagram , Facebook na wanapenda sana YouTube.

Hapo ukitaka uuone moto wa wabongo wachokoze kwenye hizo platforms, hata wasanii wengi wa bongo wanafanya promo za kazi zao katika maeneo hayo matatu.


Platforms kama twitter na zile za kustream miziki kama spotify na apple music wabongo wengi hawatumii na wengine hawazijui.


Kenya wanatutania sana kule twitter , ila hawathubutu asilani kuleta ligi Instagram maana kule ndio wabongo wengi wapo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…