Wasanii wa East Africa Bado Ni Local Champions, Beyonce awatosa

Wabongo wengi wakiona mtu kafikisha views milioni 1 kwa siku na tranding 1 YouTube wanaona Tayari wimbo umefanikiwa kumbe hawajui YouTube Ni part ndogo Sana ya kufanikiwa kuupeleka mziki mbali
 
Kabisa wabongo Ni wagumu kuelewa Sana
Naona wameanzisha movement na kumtagi Beyonce awakumbuke
 
Hizo show Ni nothing kwa ukubwa wa Diamond kwa Sasa miaka 3 nyuma alikuwa anafanya kwa level hiyo maana yake amestack pale pale.
Kwasasa tulitakiwa kumuona kwenye Big stage Kama Summer Jam na Coachella.
Diamond hajaanza kuwa na show nyingi za aina hiyo mwaka huu
 
Wabongo wengi wakiona mtu kafikisha views milioni 1 kwa siku na tranding 1 YouTube wanaona Tayari wimbo umefanikiwa kumbe hawajui YouTube Ni part ndogo Sana ya kufanikiwa kuupeleka mziki mbali

Kweli kabisa YouTube na Instagram ni part ndogo sana kwene Music Industry duniani ikumbukwe hivi vitu kuna inchi haziruhusiwi na huwez ona Insta wala youtube...kuna mambo mengi sana hapo katikati kama maredio na nini...
 
Msanii kama diamond alikua ameshafika mahali fulani. Sijui akabweteka au ndio kiki zimezidi. Angekua mbali zaidi yani ni kama amerudi hatua 10 nyuma.
Halafu kingine wenzetu west wanashirikiana huku kila mtu anataka awe juu ya mwenzie na kushushana.
 
NI RAHISI KUFKA MBALI UKIENDA PEKE AKO MAANA HAKUNA MAKELELE, LAKINI NI RAHISI ZAIDI KUFIKA MBALI ZAIDI UKIWA NA WENZAKO, UKWELI MCHUNGU NI KUWA USHIRIKIANO WA WASANII WA BONGOFLEVA WAO KAMA WAO UPO KIMAKUNDI MAKUNDI, LAKINI HAKIMU WA JAMBO HILI NI MASHABIKI WA MZIKI HUU, TOFAUTI HII NI KUBWA KULINGANISHA NA WASANII WA NIGERIA, WANAPEANA SUPPORT KWENYW KILA HATUA NDIO MAANA WAKO WENGI SANA KTK SOKO LA KIMATAIFA(😂😂😂🙌🏼🙌🏼🙌🏼🙌🏼🙌🏼🙌🏼)
TATIZO LA WASANII WA BONGO NA MASHABIKI UCHWARA NI KUTAKA KIMATAIFA AWEPO AMA WAWEPO WASANII WAWILI AMA WATATU!!! HILO LA KUSEMA TUNAPELEKA MUZIKI WETU KIMATAIFA ZAIDI ITACHUKUA KARNE KIDOGO KUFIKA HUKO, UNDERGROUND WANGAPI WANAJITAHIDI KUFKA JUU LAKINI MASHABIKI WANAZIBA MASIKIO KANA KWAMBA HUU MZIKI NI KAMA CR7 NA MESSI KTK BALOON D'OR, RAIA SHAZI MTAANI WANAKUFA NA TALANTA ZAO ILA KISA TU HUU UPEPO WA KUPENDA SAUTI MBILI KTK SIMU YAKO INAZIMA TALANTA ZAO, IFIKE WAKATI MASHABIKI WAWE WAWAZI NA WAFUNGUE MIOYO KURUHUSU KUWAPOKEA WASANII WAPY KTK VICHWA VYAO, KATI YA WATU AMA MARAFIKI KUMI ULIONAO KUNA MMOJA AMA WAWILI NI WASANII JE USHAWAHI JIULIZA TALANTA YAKE INAPOTEA VIPU LICHA YA KWAMBA ANAPAMBANA KUTWA NA USIKU KUFIKA PALE ANAPOPAOTA KUFIKA?? TUSITEGEMEE KUTEKA SOKA AMA KUSIKIKA KIMATAIFA KWA MTINDO TUNAVYOENDESHA MUZIKI HUU WA BONGI FLEVA,
It shall never come if the Tanzania musician and Fans cant change their habit.
 
Ile slogan ya hakuna matata, na ya simba kaitoa wapi? Kwa sababu kiswahili ni mali yetu huyo promotor alifanya uteuzi ni mwizi
 
Mkuu fafanua huyu akijana wetu afanyeje ili awepo huko kwenye hayo ma tidal sijui??
binafsi sijui chochote kuhusiana na hayo mambo
 
Mkuu fafanua huyu akijana wetu afanyeje ili awepo huko kwenye hayo ma tidal sijui??
binafsi sijui chochote kuhusiana na hayo mambo

Kusema ukweli diamond anajitahid sana ila sisi hapa hatuna watu wenye ushawish uko kwene mainstream kubwa na ndio wanapotupiga gep wanaija wanamajitu yao huko yanawapush sana watu wa kwao hata kama wewe leo hii ungekuwa wewe ndio upo huko lazima ungepush cha nyumbani mkuu, hili ni tatizo pia, kwa hapa hatuna cha kufanya kwakweli kijana kashapambania kombe sana wala sio wakulaumiwa kabisa, ila pia instagram na youtube zinatutanganya na kutufanya turidhike sana..Ulaya na Marekani majitu ya west Africa kwa afrika ndio yamekaba pande zote, unakuta Tv nyingi za mziki yan zile Tv kubwa za Mziki Afrika wakurugenz karibia wote Wanaija so obviously watapendelea watu wa kwao yan ni hivyo tu...
 
Mambo yake muachieni mwenyewe huyo Beyonce...

Hizo zote ni fitna kutoka kwa Trump...



Cc: mahondaw
 
Tatizo kubwa ni kuwa mziki wa hawa wasanii wetu ni wa kuiga na siyo wa asili yetu. Na cha kuiga siku zote kiwango chako kisipokuwa cha juu kama au zaidi ya wale watu wanaowaiga basi ujue una shada kubwa. Ukichukuwa mwanamziki kama Diamond unakuta kuna malaki na malaki ya wanamuziki duniani wanaopiga muziki mzuri kuliko yeye mara kumi. Ni lini atajulikana kama siyo kujifarahisha na soko la Bongo tu. Tunatakiwa tuwe na muziki wetu hapo ndiyo tunaweza kuwashawishi watu kusikiliza kitu wasichokijua.
 
kuna kondoo mmoja nilikutana naye alinikera sana,nikahitimisha kumbe ndio maana hata wasanii wetu hawaendelei zaidi ya walipo sababu ya vichwa utomvu kama huyo jamaa.

ananambia kwa sasa kimuziki,diamond anapitwa na davido tu,kaenda canada,jamaica,na marekani kajaza uwanja wa mpira,yeye ameona youtube[emoji34][emoji34][emoji34].
 
Hapana kaka. Sikuhizi mambo yamebadilika sana na mziki umekuwa biashara kama biashara nyingine. Hivyo basi ushawishi na 'marketing strategy' ndio msingi wa kujulikana. Jay Z akiamuwa kuiga mziki wa Kipuertorico, Salsa au Charanga, yeye na menagement yake wakausukuma mbele, atauza sana sana. Sababu tu Jay Z ana ushawishi na usambazaji mzuri wa sanaa yake. Na wanamziki wengi wataanza kupiga aina hiyo ya muziki. Lakini ukiangalia huo mziki hauna asili ya Jay Z. Kwahiyo si kweli kwamba Diamond inabidi afanye mziki wa kwao ndio atauza au kuwa maarufu. Dunia ya leo watu wanataka burudani tu, pia ukiangalia kwa karibu utakuta si burudani. Watu wanafuata mkumbo au 'trend'.
Hivi sasa huku mitandaoni Watanzania wanahasira kwelikweli. Wamemkalia kooni Dada Beyonce. Kwanini kafanya album ya Tanzania, Serengeti. Beyonce kaimba mpaka maneno ya Kiswahili, lakini kwenye album kawashirikisha Wanaijeria watupu. Hakuna hata wa East Afrika mmoja. Watu wanakomaa nae huko, kwanini kafanya hivyo.
Waswahili tunasema 'kisichopo machoni na moyoni hakipo'. Pamoja na matatizo mengine ya Serekali kuwa nyuma kwenye kuitangaza Tanzania, pia Wanaijeria ndio walipenya zamani kwenye soko la nje ya Afrika.
 
Mwanzon Diamond aliwatishia Wanaijeria kwa mbaliii,Wakaona Dawa yake ni kumpa makolabo mengi,walivyo maliza hyo Dawa wakawa wame maliza kila kitu cha Diamond kwenye soko lao,Saiv hawana habari naye cz nw siyo levo yao tena,Harmonize tena naona hvo hvo makolabo mengi ila cha ajabu wasanii wetu hawashituk.
 
Ni kweli wasanii wa East Africa ni local champion.Lakini hata hivyo Beyonce sio kigezo Cha kupima kiwango Cha msanii kuwa wa kimataifa.

Kwani yeye Beyonce nani mpaka atukoseshe raha.Halafu tusimpangie jinsi ya kufanya kazi zake.
 

Mkuu tofauti ni revenue generating capacity...W/Africa ina potential ya ku generate revenue kuzidi E/Africa.....ni hilo tu!
 

Naomba uweke TICK kwenye sehemu atakazo enda....nakuhakikishia ataishia kwenye show za Wasafi Festival tu na Essence.....kijana ana mbwembwe za ki zamani....hizo style za kuji overrate zishapitwa na wakati
 
Naomba uweke TICK kwenye sehemu atakazo enda....nakuhakikishia ataishia kwenye show za Wasafi Festival tu na Essence.....kijana ana mbwembwe za ki zamani....hizo style za kuji overrate zishapitwa na wakati
Nishakujua wewe mziki ujui au ufatilii mzee baba diamond kila akienda show za nje anafanya maukumbi makubwa na zingine uwanjani na amekuwa akijaza na Mara nyingi show zake zinarushwa wasafi tv na pia zingine zirushwa live na za hizo nchi mzee baba wewe unaishi dunia ipi? na sometimes anarusha live YouTube mzee baba inamaana ujui? Je uonaji hata mapokezi makubwa anayopata kwenye hizo nchi? Sema tu wenzetu Nigeria wametuzidi cos wana wanasimamiwa na watu wenye exposure na connection kubwa global hii ndio tofauti yetu na wao lakini kuhusu kufanya vizuri mbona diamond anafanya vizuri tu angalia ngoma yake ya inama imeshika no 2 kwa kudownlodiwa Mara nyingi kwa wasanii wa africa ktk mtandao wa sportfy hata pia nimeona hata kwenye media kubwa km soundcity ngoma yake inachezwa Sana na pia wimbo wake wa kanyaga.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…