Si wasanii tu hata wasio wasanii tunakutana nao mitaani wengi wamejichubuwa.
Cha kushangaza si wanaume tu, umeshaona wanawake wanavyojichubuwa? mpaka wengine wanakuwa wa pinky sura zao. Hatari kubwa sana hii, nasikia hawa wanawake wanaojichubuwa mwili mzima hutowa harufu mbaya sana, jee ni kweli jamani?
Kama ni kweli kwa nini dada zetu wanakataa Rangi za asili alizotuumba nazo Mwenyeezi Mungu, kuna urembo wa kuzifanya ngozi ziwe nyororo na kuvutia, tena wala hauna gharama ni wa kiasili kabisa wala hauna haja ya kujichubuwa. Vitu kama asali, samli safi, vikipakwa mwilini, ngozi inakuwa na mvuto wa kipekee na nyororo na inabaki na rangi yake ya asili, tazama wasomali, hukuti wamejichubuwa lakini tazama ngozi zao zilivyokuwa laini, ni samli tu wanapaka.
Sasa na hawa wanaume tena hata sijui kwa nini? labda dili kuwa mweupe?