Ngaliba Dume
JF-Expert Member
- Oct 6, 2010
- 1,710
- 3,681
Leo katika Uwanja wa Aman Zanzibar,makamu wa kwanza wa Rais Balozi Seif Idd amezindua kampeni rasmi ya wanamuziki wa kizazi kipya watakaozunguka Tanzania nzima kuhabarisha na kuhamasisha upigaji wa Kura ya "NDIYO" kwa rasimu ya katiba iliyopendekezwa,akiongea na hadhara ya watu ktk uwanja wa Amani,Seif amewaambia Wazanzibar waipigie katiba inayopendekezwa Kura ya "NDIYO " kwani ina mambo mengi inayowafaa na kuwaletea maendeleo wao na vizazi vyao.
Akiongea kwa niaba ya wasanii waliojiunga kuipigia kampeni rasimu ya katiba mpya,NIKI awA KWANZA amesema kwa muda wa Miaka 50 toka nchi hii ipate Uhuru wasanii hawakuwahi kutambulika ktk katiba na wala kazi zao hazikuweza kutambulika kisheria,anasema katiba iliyopo ilitambua haki za Mali inayohamishika na Mali isiyohamishika lkn haikutambua mali isiyoshikika,wao kama wasanii wamejitahidi kushinikiza kuwepo na utambuzi na urasimishaji wa haki za Mali zisizoshikika kama muziki wao wa kizazi kipya,hivyo kuwasihi Wananchi wa Zanzibar waipigie Kura ya ndio katiba inayopendekezwa sababu imegusa maslahi mapana ya Watu wa makundi yote.Nikki wa Pili amemwambia Balozi Seif kuwa tasnia ya Sanaa ya muziki wa Kizazi kipya Tz ina mtaji wa Watu milion kumi,hivyo watatumia uwingi wao na nguvu yao ya kiushawishi kwa Vijana kushawishi waipigie Kura ya NDIYO katiba inayopendekezwa,kwani katiba hii imebeba matumaini na mustakabali mzuri wa Taifa na watu wake.
Wasanii waliohudhuria ufunguzi huo ni Niki wa Pili,shilole,Peter Msechu,AT,Barnaba Boy n.k...kampeni hiyo itakuwa ni ya nchi nzima ili kuwahamasisha Watanzania kupiga Kura ya NDIYO na kuepukana na maneno ya wanasiasa na viongozi wa dini walioanza kujitokeza kuhamasisha kuikataa na kuipigia Kura ya HAPANA katiba pendekezwa.Kongamano hili lilionyeshwa moja kwa moja na TBC1 na ZBC1