Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 15,101
- 56,054
Musa alikwenda na Meseji Moja tu kwa Farao, nayo ni "Let my people Go". Farao akashupaza shingo, akaangalia majeshi yake akaona hakuna mfalme kama yeye duniani.
Akaangalia wachawi wake, akasema yeyote atakeyukuja kwa hawa magwiji hatofua dafu.
Lakini sote tunafahamu mwisho wa kilichotokea, Majeshi ya Farao yalishindwa vibaya kwa Nguvu za Mungu na Wachawi wa Farao hawakumsaidia, tena wengine waliikubali meseji ya Musa.
Chama cha Mapinduzi nchini, kimejawa na kiburi cha mamlaka, Watawala wanatwambia kuwa ndani ya chama hicho kuna mijizi lakini hawachukui hatua kuishughulikia. Wanatwambia wale waliotoa rushwa kwenye kura za maoni ndani ya chama hicho hawatoteuliwa lakini cha ajabu ndiyo walioletwa mbele yetu kugombea.
Chama cha mapinduzi kimebariki kila aina ya siasa za kilaghai na ghiliba bila hofu yoyote ya wananchi kwa sababu kina majeshi kina dola.
Miaka 68 ya uhuru, hali ya maisha ya wananchi wengi nimekuwa hohehahe. Watu wanabambikiziwa kesi, mapambano ya ufisadi yamekaa kisanii wasiotakiwa wanashughulikiwa ila wale waenzetu utadhani jicho haliwaoni.
Watumishi wa umma hawapewi stahiki zao halali kwa mujibu wa sheria, huku bunge likigeuzwa kuwa kama rubber stamp. Ahadi wanazotoa majukwaani au hata kwenye ilani yenyewe baada ya muda wanazikataa!. kwa mfano Iko wapi katiba mpya?, ziko wapi milioni 50 kila kijiji?
Sasa upepo wa kisiasa umegeuka, kama Musa kwa wana wa Israel huenda Lissu ni mbeba maono wetu. Huyu kasimama toka mwanzo kabisa kupinga ulaghai wa kisiasa katika nchi hii.
Kama vile Musa alivyotaka uhuru wa wana wa Israel, Lissu anataka uhuru wa Watanzania. Uhuru anoutaka Lissu siyo ule wa bendera ambao tulishaupata toka mwaka 1961, bali huyu anataka uhuru wa kisiasa, kiuchumi, kitamaduni, kifikra, n. k
Pia Lissu anataka Haki, watu wasibambikiziwe kesi, wafanyabiashara wasiporwe utajiri wao, wakulima wasinyanyaswe kwenye mazao yao n. k
Pia anataka Maendeleo ya watu.
Sasa katika hali kama hiyo, kama vile Farao alivyoamini kuwa Wachawi wangemsaidia dhidi ya ujumbe wa Musa, ndivyo hivyo Magufuli anavyodhani Wasanii wa muziki kwenye kampeni zake watamsaidia!.
Mimi nasema hivi, Siyo wasanii wala viongozi wa dini maslahi watakaomsaidia safari hii, Meseji ya Lissu ya uhuru, haki na maendeleo ni meseji nzito sana, Wananchi wanaielewa!
Binadamu haishi kwa vitu tu bali uhuru pia.
Leo hii ukimchukua paka ukampa kila aina ya msosi mzuri lakini ukamnyima uhuru, ipo siku atatoroka aende huko barabarani akaungane na mapaka mengine, aishi kwa kujitafutia mwenyewe hata majalalani lakini ilimradi awe huru!. Kama hali iko hivi kwa viumbe wengine je kwa binadamu je?
UHURU, HAKI, MAENDELEO!