Wasanii wa Tamthilia ya Mawio watembelea ubalozi wa Tanzania Comoro

Wasanii wa Tamthilia ya Mawio watembelea ubalozi wa Tanzania Comoro

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,278
Reaction score
797
Wasanii wa tamthilia maarufu ya Mawio nchini Tanzania Gabo, Barnaba na Sarah leo wametembelea Ubalozi wa Tanzania nchini Comoro na kupokewa na Mhe. Balozi Saidi Yakubu.

Wasanii hao walioongozwa na Gabo wamemueleza Balozi Yakubu wapo Comoro kwa kuwa tamthilia yao ina mashabiki wengi Comoro na hivyo wameamua kurekodi kipande kidogo kisiwani Ngazidja.

Kwa upande wake Balozi Yakubu aliwapongeza kwa hatua hiyo na kuwaeleza kuwa kufanya hivyo kunaongeza ushirikiano na udugu wa kihistoria wa Tanzania na Comoro hususan kwa kuwa kipande hicho kimeshirikisha wacomoro pia.

Katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Watanzania nchini Comoro, Robert Shirima alishiriki.

IMG-20240925-WA0331.jpg
IMG-20240925-WA0328.jpg

IMG-20240925-WA0330.jpg
 

Attachments

  • IMG-20240925-WA0334.jpg
    IMG-20240925-WA0334.jpg
    96.9 KB · Views: 3
  • IMG-20240925-WA0329.jpg
    IMG-20240925-WA0329.jpg
    103.1 KB · Views: 3
  • IMG-20240925-WA0331.jpg
    IMG-20240925-WA0331.jpg
    107.1 KB · Views: 3
Back
Top Bottom