Wasanii wa Tanzania wazua balaa Kenya, washushwa jukwaani na kupewa onyo kali

real G

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2013
Posts
5,227
Reaction score
5,299
Kundi la wasanii wa muziki wa Tanzania kutoka visiwani Zanzibar, Off Side Trick, wamesababisha kufungwa kwa tamasha la utamaduni la Lamu huko Mombasa nchini Kenya, baada ya kucheza mtindo usiofaa wenye kukiuka maadili.

23659289_2175696679111405_8102114935908603878_n.jpg

aarifa kutoka Mombasa zinasema kwamba kitendo hiko kililalamikiwa na wakazi wa eneo hilo, viongozi wa dini na viongozi wa utamaduni wa Kenya, baada ya kuangalia kile kilichokuwa kikiendelea jukwaani na kulazimu tamasha hilo kufungwa.

Baadhi ya watu walijaribu kuwaonya kundi hilo kuacha kucheza michezo hiyo ya uchafu ambayo sio maadili lakini walijifanya kutosikia, na ndipo waandaaji wa tamasha na viongozi wa eneo hilo kupanda jukwaani na kuwashusha kwa nguvu .

Baada ya tukio hilo Mkurugenzi Msaidizi wa Nyumba ya Maonyesho wa Kenya, Bwana Athman Hussein, amesema kuna haja ya kuwahakiki wasanii kabla hawajapanda jukwaani, kwani kitendo hiko kimedhalilisha jamii ya hapo na mji wa Lamu kiujumla, kwani mji huo ni maarufu kwa utalii na pia uko chini ya Urithi wa dunia wa UNESCO.

Video

Chanzo: EATV
 
Acha waisome ya Uhuru Kenyatta anayomsomesha RAO huko kwenye NASA.
 
Hivi hiki kikundi bado tu kipo? Hakifai hata! Kimekaa kishogashoga zaidi,kafutwe tu!
 
Kundi la wasanii wa muziki wa Tanzania kutoka visiwani Zanzibar, Off Side Trick, wamesababisha kufungwa kwa tamasha la utamaduni la Lamu huko Mombasa nchini Kenya, baada ya kucheza mtindo usiofaa wenye kukiuka maadili.

View attachment 635143

aarifa kutoka Mombasa zinasema kwamba kitendo hiko kililalamikiwa na wakazi wa eneo hilo, viongozi wa dini na viongozi wa utamaduni wa Kenya, baada ya kuangalia kile kilichokuwa kikiendelea jukwaani na kulazimu tamasha hilo kufungwa.

Baadhi ya watu walijaribu kuwaonya kundi hilo kuacha kucheza michezo hiyo ya uchafu ambayo sio maadili lakini walijifanya kutosikia, na ndipo waandaaji wa tamasha na viongozi wa eneo hilo kupanda jukwaani na kuwashusha kwa nguvu .

Baada ya tukio hilo Mkurugenzi Msaidizi wa Nyumba ya Maonyesho wa Kenya, Bwana Athman Hussein, amesema kuna haja ya kuwahakiki wasanii kabla hawajapanda jukwaani, kwani kitendo hiko kimedhalilisha jamii ya hapo na mji wa Lamu kiujumla, kwani mji huo ni maarufu kwa utalii na pia uko chini ya Urithi wa dunia wa UNESCO.

Video

Chanzo: EATV

Hawana lolote hawa watu walamu,hata Zanzibar mji mkongwe uko chini ya urithi wa dunia wa UNESCO,sasa UNESCO inahusiana nini na huu ushamba wa watu wa Lamu.

Hichi ni kikundi cha kisanii hakikwenda Lamu kuimba kwaya au kusoma kasida kimekwenda Lamu kuonyesha mitindo ya mziki wao kila mtu na maadili yake,tunawaona wasaniii wengi tu wanapanda kwenye majukwa na vichupi mbona hatujayasikia haya..
 
Hivi kumbe wamo Ila Kenya sijui hawajui mziki wanapenda magarasa ya kibongo hao hata uwaweke leaders waimbe bure haendi mtu nakumbuka walimchukua Mr Nice pia
 
Kumbe Kenya biashara inalipa...hilo kundi nilijua lishajifia kifo cha mende duuh
 
We unawaita ilo kundi wana nyimbo inaitwa bata...tena bata la katikati lenye nyama laini...unategeea kuona nn apo..mmeyataka wnyw
 
Naona hawa jirani bado wana hasira ya kuchomewa Vifaranga wao
 
Back
Top Bottom