Wasanii wa Wasafi washinda Tuzo Saba usiku mmoja katika East Africa Magic Vibes Awards

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Wasanii wa lebo ya muziki, Wasafi Classic Baby (WCB) wameendelea kuthibitisha ubora wao kwenye soko la muziki baada ya kushinda jumla ya tuzo saba kwenye 'East Africa Magic Vibes Awards' usiku wa kuamkia leo Desemba 16. Ushindi huu ni wa kihistoria kwa lebo hiyo inayotambulika kwa kuwatengeneza wasanii wakubwa Tanzania.

Hizi ndizo tuzo walizoshinda:

1. The East African Giant - Diamond Platnumz
2. Best East African Live Act - Diamond Platnumz
3. Best East African Music Video - Komasava Remix ya Diamond Platnumz
4. Best East African Collaboration - Komasava Remix ya Diamond Platnumz
5. Best East African Male R&B & Pop Artist - Mbosso
6. Best East African Female R&B & Pop Artist - Zuchu
7. Album of the Year - Swahili Kid ya D-Voice

Kupitia ukurasa wao wa Instagram, WCB walieleza shukrani kwa waandaaji wa tuzo hizo pamoja na mashabiki waliowapigia kura.

 
Hiyo ya saba ndo imepigilia msumari ile nadharia ya huwa zinanunulika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…