Nadhani tatizo halipo kwa wasanii bali kwenu mnaowaona wao ni wa kuigwa kwakuwa tu "Ni watu maarufu"
Kioo kazi yake ni kuonyesha taswira, na kusema msanii ni kioo cha jamii inamaana tunapowaangalia wasanii tunapata kuona mazuri na mabaya ya jamii yetu..
Sidhani kama kuna kioo unachoangalia kinachokuonyesha upo safi usoni na kuzificha chunusi na michirizi wakati ipo..
Ndio maana kutofautisha viumbe wengine na binadamu, MUNGU ametupatia "akili na utashi" tuyatambue mazuri na mabaya kabla ya kuamua kuyafuata, kwahiyo kazi kwenu mnaoangalia "Gigy Money" kafanya nini ili muige...!!