Lavit
JF-Expert Member
- May 16, 2011
- 14,834
- 32,522
Itoshe tu kusema kwamba muziki wa Bongo Fleva umekua na kufika mbali pengine tofauti na ilivyofikiriwa...
Miaka ya mwanzoni ya 90 huu muziki ulionekana ni wa kihuni tu, huku muziki wa Congo ukitamba, baadaye muziki wa taarabu na hata dansi mwanzoni mwa miaka ya 2000...
Katika miaka yote kumetokea wasanii wakubwa ambao waliweza kusumbua vilivyo...na wengine walikosa kabisa upinzani...
(1995-2000)-Katika kipindi hiki utawala ulikuwa wa 2proud ambaye baadaye alikuja kujiita Mr II aka Sugu...Katika kipindi chake ni kama kulikuwa hamna upinzani wowote...ni yeye pekee aliyefanikiwa kutoa album kila mwaka na kufanya mauzo karibia nchi nzima. Albamu kama Ndani ya Bongo, Nje Ya Bongo, Millennia na hata Muziki na Maisha ya mwaka 2001 ilifanya mauzo ya kutosha....
(2000-2005) Hapa ukiachilia mbali makundi ya muziki yenye umaarufu mkubwa kama Wateule, TMK, ECT na hata HBC, kuliibuka manguli wengi katika sanaa .
Hapa kulikuwa na Prof J, Jay Moe, Juma Nature, Afande Sele, Mwanafa na AY kwa upande wa Hip Hop/Rap. Kwa upande wa miziki ya kuimba alikuwepo TID,Mr Nice, Dully na wengine...
Hiki ni kipindi kilichoshuudia upinzani mkali sana, huku wengine wakiona J ndo mwenye kustahili ufalme, wengine wakimtaja Sir Nature, na wengine Mr Nice Akiwa amebaki kwenye kumbukumbu zao...
Japo Ufalme wa Rhymes wa 2004 uliitimisha kwamba Sele ndiye mkali, wengi hawakukubaliana na hilo...
Je ni nani alikuwa namba 1 katika kipindi cha hiki???
(2005-2010)
Hapa kuliibuka kundi kubwa sana la wasanii wanaoimba almaarufu kama Wabana Pua. Hiki ndicho kipindi tulichowashuhudia akina Alikiba,Marlaw na Matonya wakiwa wanahit na kazi zao mbalimbali...
Wengi wanamtaja Alikiba kama ndiye mfalme katika kipindi hicho...
2010-2015...
Hiki ni kipindi ambacho muziki ulienda mbali zaidi huku wengine wakilalamika muziki kupoteza ladha na kuingiza unaijeria mwingi.
Hapa napo wasanii kama Diamond, Ommy Dimpoz,Vanessa na Rich Mavoko walionesha uwezo wao.
Diamond amekuwa akitajwa kama msanii namba moja mpka hivi sasa, huku akionekana kukosa mshindani wa karibu kama ilivyokuwa katika vipindi vya nyumba.
Je ni msanii gani atafata Baada ya Diamond???