Wasanii wanaofanya muziki bila kuwa na dira wala mwelekeo

kanali mstaafu

JF-Expert Member
Joined
May 17, 2015
Posts
4,318
Reaction score
4,105
Izzo busness, Stamina, Country boy, Quick rocka, Baba levo, Ali kiba, Nuh mziwanda, Gigy Money, Shetta na Kimbunga mchawi..

Sasa nimeanza kuamini kauli ya nguli wa muziki wa Hip hop, Juma Mchopanga almaarufu Jay Mo..

"Siku hizi msanii anaweza kufanikiwa kutokana na kuwa ktk mainstream, lkn kazi zake zikawa hazina ubunifu wala kitu kipya kinachokupa morali wa kusikiliza huo wimbo zaidi ya mara moja".

Wasanii tajwa hapo juu wanafanya tu mziki kwa sababu wana ujasiri wa kwenda kwny booth na kupaaza sauti kisha wanatoa hela kwa prodyuza wanaondoka wanasubiri zali...

Muziki wa wasanii hao tajwa upo upo tu na wanaimbaimba tu hawana dira halafu wanatujazia idadi ya wasanii hewa....

Nashauri wawe serious na pia wajue wanachokifanya.
 
Umewasahau Lady JayDee, Diamond, Mpoto, Isha Mashauzi na Le Mutuz.
 
Hahahahaha nimecheka mbele za watu mpaka wamenishangaaa et le mutuz
 
Kwanini umemtaja Gigy Money bila ya Partner wake mzee wa Tembo?
 
haa haa watu mnautani wa vita..hadi le baharia? ...
ila sio fair unamuwekaje ali k na gigi mahela kundi moja?
 
uuuiiwiiiiii balaaaa hili ukiamka usome ulichoandika utangundua makosa yako
 
Mainstream sio kuingia studio na kurekodi, main stream ni kupata fluent consistent airplay hiyo ndiyo ilikua maana ya J Moe
 

Ungeanza na kala pina ningekuelewa sana!..
 
Hizo chuki zako kwa king wa muziki bongo hazitakufikisha popote ndugu
 
mtoa mada una maana kubwa sana,wachache ndiyo watakuelewa...mwongeze na isha mashauzi,snura
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…