wasanii wetu jamaanii!!!!.

wasanii wetu jamaanii!!!!.

ngoshwe

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2009
Posts
4,131
Reaction score
937
Msanii anapofikiria kwa Kiswahili ili kuongea Kiingereza


Jameni..Jameniee, pengine tunahitaji kulazimisha tu kutumia lugha yetu ya kiswahili kama ilivyo kwa baadhi ya mataifa mengine. Wasanii wa Kitanzania walio wengi wanafanya vizuri lakini pale inapokuwa kwa suala la lugha. hususani hii inayoitwa lugha ya "biashara na ya Kimataifa" ya Kiingereza...mh, .tabu tupu na pengine labda ndo inatukosesha biashara au kutambulika katika kazi zetu za mikono na akili zetu kama si kututia aibu kwa mataifa mengine na kuonekana tuna babaisha kwenye mambo yale tunayosema tunayajua kisa tu ni kushindwa kujieleza ipasavyo kwa lugha ya kigeni....

Ebu sikiliza huyu Msanii wa Uchora na Uchongaji ( Heindrick Lilanga), mjukuu wa Hayati George Lilanga, anavyoumiza akili kutafuta maneno ya kuchomeka katika mawasiliano iliaweze tu kueleweka kwa muthungu na kushindwa kuweleza mthungu moja kwa moja kuwa "yeye hajui kiingereza ili mthungu amtafute mkarimani wa kutafsiri mahojiano yao!"..


Ni kama yale yale ya BBA ya "mzee wa ZE WORLD" (S.K).






Yu siiiiiii.....







Pata Habari kamili kuhusu utata wa umiliki asilia wa kazi za sanaaa za Marehemu George Lilanga hapa

http://www.lilanga.org/lilanga_artists.html
 
Last edited by a moderator:
Haaa! Ung'eng'e kwa hakika ni mtihani mgumu: maana jamaa anahangaika sana. Hakika yafaa tuongee Kiswahili chetu tu. Ung'eng'eni si kwetu.
 
Na hapo anataka auze kazi zake kwa MUthungu kupitia jina la Marehemu Babu yake (as Only remained genuine Lilanga). Maumivu si kidogo kwenye hii lugha .........kazi kazi!!.
 
Msisitizo jameni- na kikazi zaidi!...msisahau hilo!
 
Huyu jamaa anasthili sifa ana-deliver message na confidence ya hali ya juu na message yake iko very clear.

Tatizo la wa TZ nikukosa kujiamini na inferiority walizo nazo na pia kurudishana nyuma, na dhani ni ukosefu wa international exposure, kama wangeelewa wako wengi duniani wanafanya biasha za juu na pia wanasiasa, wawakilishi wa jumuia nao pia wana struggle kwenye kutumia lugha za watu wengine, chamsing zaidi ni kwamba message delivered.

Wakina M7, Kinyata, na wengineo mnaofikiria wanajua english wote hao wanaboronga, wanaongea english utafikiri ni kilugha chao, hakina grammer nk.

Tuachane na tabia ya kuchekana, wako wengi duniani wasio jua english na bado wana delver message. Tuachane na inferiority complex. Thanx
 
Back
Top Bottom