MakinikiA
JF-Expert Member
- Jun 7, 2017
- 5,104
- 6,827
Bilionea rafiki wa Putin: Ni wakati wa kuwaonyesha Magharibi nguvu za kijeshi za Urusi
Mmoja wa watu wenye ushawishi mkubwa wanaounga mkono uamuzi Vladimir Putin wakuivamia Ukraine mwenye jumri wa miaka 71 Yuri Kovalchuk, amesema kuwa vita inaweza kuonyesha uthabiti wa Urusi kwa nchi za Magharibi. Bilionea Kovalchuk, ameyasema hayo katika Makala ndefu ya jarida Wall Street.
Nchini za Magharibi ni dhaifu na muda umefika kwa Urusi kuonyesha nguvu zake za kijeshi kwa kuivamia Ukraine, alinukuliwa na vyanzombali mbali vya habari magazeti ya Marekani, akisema .
Mara kwa mara amekuwa akikutana na Putin kabla vita vya Ukraine havijaanza, na pia amekuwa akizungumza naye kwa njia ya simu na video.
Kovalchuk, ambaye aliwekewa vikwazo mwaka 2014, ni mfanyabiashara anayemiliki kampuni ya habari - yenye vituo vya TV, magazeti, mitandao ya kijami inayounga mkono utawala wa Urusi.