Washabiki wa Yanga walivyo maboya, wameaminishwa Simba ni mbovu wakasahau kuwa wametolewa klabu bingwa

kibaravumba

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2012
Posts
6,634
Reaction score
7,015
Kwa sasa wanaamini kwa vile wamesajili wacongo wengi basi TP Mazembe imewawakilisha.

Ninashangaa wana furaha sana licha ya kutolewa klabu bingwa Afrika mechi ya awali kabisa. Wao wanaamini kikosi chao kina uwezo wa kuifunga Simba.

Nahisi wengi wanafikiri eidha nao walikuwa wanacheza mechi ya kirafiki ama walidhani Simba naye amecheza mechi ya klabu bingwa.

Kama ni kufurahia Simba kupoteza kwa vile wao pia walipoteza na Simba ikafurahi, wajue tu kuwa wanasimba walifurahi kutokana na mfungaji wa goli siku ile; Muhimu sana kumkumbuka "Kapumbu"
 
Mbona matusi ghafla mtani. Maana ulikuwa mzima tu wa akili asubuhi.

Kwani unaonaje kikosi chako ambacho MO anasema ni bora kuliko cha Chama na Miqquisone?
 
Uko sahihi kabisa, yani endapo simba leo angeshinda japo bonanza na wao leo wamepoteza basi kingewaka Kule utopoloni,, ila kwa kuwa simba wamefungwa leo basi na wataaminishwa na viongozi wao kuwa simba mbovu na watasahau kama wametolewa
 
Jipe moyo lkn hamna timu pale...
 
Hawa jamaa akili zao wanazijua wenyewe, eti wanafananisha Necta na Kwizi
 
Furaha ya Yanga kwa sasa ni kama Simba inafungwa na Yanga au timu nyingine.
Furaha ya Simba kwa sasa ni kuona Simba inashinda mechi za Kimataifa.

Ni kwamba tupo levels tofauti, wenzetu ni wa hapa hapa.
Na wanafurahia mambo ya hapa hapa.
 
Kwa sasa wanaamini kwa vile wamesajili wacongo wengi basi TP Mazembe imewawakilisha.

Ninashangaa wana furaha sana licha ya kutolewa klabu bingwa Afrika mechi ya awali kabisa. Wao wanaamini kikosi chao kina uwezo wa kuifunga Simba...
Umekuwaje mkuu mbona unapaniki tatizo nini, majigambo yenu ndo yamewarudia na timu yenu kali tumeiona bwana, tulia kunywa maji mengi upumzike ee bwana,,,mko vizuri Sana yani mkuu🤣🤣🤣🤣🤣
 
warudi kwenye kazi ya kawaida ya kupokea timu zinazokuja kucheza na Simba na kuwaaminisha uongo tumepuliza dawa kwenye vyumba vya wachezaji
 
Wewe mwenyewe kwenye nafasi yako Simba umeionaje?
 
Aisee Simba hadi mashabiki wamevurugwa. Aliyemuelewa huyu anisaidie nami nielewe
 
Makolo mmevurugwa soon mtavua nguo.Sasa hapa umeandika nini??😆😆
 
Ndo haya wanasema usitukane mamba kabla hujavuka mto, usitukane wakunga na uzazi ungalipo. Haya mzee wa klabu bingwa kiko wapi?
 

Wakati mwingine sisi mashabiki wa hizi club mbili ni kama mapacha au watoto waliofuatana.

Tuandaliwe kongamano la kukanyaga Mafuta hahaha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…