Washambuliaji wa soka wa zamani wa kitanzania? Ni kitu gani walifanikiwa maana kumekuwa na kasumba washambuliaji wa sasa wa Kitanzania hamna kitu!

Washambuliaji wa soka wa zamani wa kitanzania? Ni kitu gani walifanikiwa maana kumekuwa na kasumba washambuliaji wa sasa wa Kitanzania hamna kitu!

barafuyamoto

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2014
Posts
32,378
Reaction score
29,739
Habari zenu!

Nilikuwa nasikiliza na kuangalia kipindi cha mshike mshike cha azam tv, leo tarehe 19/04/2019.
Wanaongelea washambuliaji wa zamani wa kitanzania.

Wamemuhoji Mogella Zamoyoni na Edibily lunyamila na madaraka suleiman Wametoa pia reference ya Mohamed hussein wa yanga kuwa hapo zamani kulikuwaga na washa mbuliaji kweli kweli wa soka hapa tanzania. Hata hao waliohojiwa wamedai ni kweli, enzi zao na pia wao wenyewe walikuwa balaa.

Sasa hivi hamna washambuliaji kabisa ambao ni wazawa wa ndani.

Swali langu: Je hao washambuliaji wa zamani ni kitu gani walifanikiwa kufanikiwa eidha ktk club au timu ya taifa Ambacho kinawafanya waamini zamani kulikuwa na washambuliaji wakali kuliko sasa?
 
Sio washambuliaji tu kwa ujumla viwango vya wachezaji wetu wa sasa kama ni muhenga waweza kunielewa vinatia shaka sana uwezo binafsi na timu pia hakuna uwiano. Japo ukianza kusema vijana wa dot com watakwambia walifanya nini na kuleta kombe gani? lakini kifupi mtuulikuwa waweza kwenda taifa (shamba la bibi ) ukajiwekea kautaratibu ka kuangalia vita pale kati ya Viungo kama kassa musa ali maumba huku issa athuman na hassan China panakuwaje? Siku hizi hata hamu huna.
 
Ni ATHUMANI CHINA mkuu,,sio HASSAN CHINA,,, huku SIMBA KULIKUWA NA RAMADHANI LENY,,HAMISI GAGA,,NICO NJOHOLE,,,ZAMOYONI MOGELA,,,EDWARD CHUMILA,,.ADAM SABU,,,nk...LEO MCHEZAJI anacheza KIUNGO HATA CONTROL BALL HANA,,,mchezaji ni MSHAMBULIAJI LAKINI hata SHOOT ON TARGET hajuwi..kwnza wachezajj wa zamani walikuwa na MAUMBO MAKUBWA SN...KULIKO SASA vijototo vitupu
Sio washambuliaji tu kwa ujumla viwango vya wachezaji wetu wa sasa kama ni muhenga waweza kunielewa vinatia shaka sana uwezo binafsi na timu pia hakuna uwiano. Japo ukianza kusema vijana wa dot com watakwambia walifanya nini na kuleta kombe gani? lakini kifupi mtuulikuwa waweza kwenda taifa (shamba la bibi )ukajiwekea kautaratibu ka kuangalia vita pale kati ya Viungo kama kassa musa ali maumba huku issa athuman na hassan China panakuwaje? siku hizi hata hamu huna

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kilichozuia wachezaji wa Tanzania kwenda nje hasa Ulaya wakati ule ni lack of exposure na siasa na sera za nchi ila ki uwezo hawa wachezaji wa sasa hawawafikii kabisa.

Kuna wakati naona kama viwango vya wachezaji wa baadhi ya timu za Premier League ni kama viwango vya wachezaji wa UMISETA wa miaka ya nyuma
 
Tazama Simba, Yanga na Azam inavyohaha kutafuta washambuliaji wa kigeni. ligi yetu kwa miaka mitatu sasa mfungaji bora anatoka nje. kifupi kwa sasa bongo vipaji ni vya kawaida sana havisisimui.

Wakati nasoma msingi kwetu kwenye timu za mtaani kulikuwa na watu wana vipaji hasa,ambapo nikitazama hawa wachezaji wa ligi kuu hawana tofauti sana.
 
Ni ATHUMANI CHINA mkuu,,sio HASSAN CHINA,,, huku SIMBA KULIKUWA NA RAMADHANI LENY,,HAMISI GAGA,,NICO NJOHOLE,,,ZAMOYONI MOGELA,,,EDWARD CHUMILA,,.ADAM SABU,,,nk...LEO MCHEZAJI anacheza KIUNGO HATA CONTROL BALL HANA,,,mchezaji ni MSHAMBULIAJI LAKINI hata SHOOT ON TARGET hajuwi..kwnza wachezajj wa zamani walikuwa na MAUMBO MAKUBWA SN...KULIKO SASA vijototo vitupu

Sent using Jamii Forums mobile app
Yaah mdogo wake ndio hassan kifupi msisimko na mashamsham hakuna ingawa walicheza hiari ya moyo kwa mavuno na vifaa hafifu pia viwanja vibovu bado walicheza kwa umahiri mkubwa. Ile michezo yetu ya danadana elfu 3 iliweza kutengeneza viungo wazuri achilia mbali handsball (henziboli )uliweza kutengeneza walinda milango bora na pia wapiga mashuti hodari ule mchezo wa kona uliweza kuzalisha wapiga vichwa hodari kama abeid Mziba (Tekelo )sasa viwanja vya wazihakuna pamerithiwa na miradi kama kumbi za vileo na makazi ya watu wenetu wanacheza game za luningani aah
 
Kilichozuia wachezaji wa Tanzania kwenda nje hasa Ulaya wakati ule ni lack of exposure na siasa na sera za nchi ila ki uwezo hawa wachezaji wa sasa hawawafikii kabisa.

Kuna wakati naona kama viwango vya wachezaji wa baadhi ya timu za Premier League ni kama viwango vya wachezaji wa UMISETA wa miaka ya nyuma
Umiseta? Umeishushia hadhi michezo hiyo au umewapendelea wachezaji wa sasa kiwango chao ni ligi daraja la nne la waqt ule nilibahatika kushiriki michezo ya umisseta waqt ule najaribu kuvuta kumbukumbu hapana kwanza nyota wengi walio tamba kipindi hicho walikuwa wamepikwa na michezo hiyo sina haja ya kuvitaja vipaji lukuki ambao ni zao la umisseta ilikuwa ni kisima cha vipaji na burudani.
 
Yaah mdogo wake ndio hassan kifupi msisimko na mashamsham hakuna ingawa walicheza hiari ya moyo kwa mavuno na vifaa hafifu pia viwanja vibovu bado walicheza kwa umahiri mkubwa. Ile michezo yetu ya danadana elfu 3 iliweza kutengeneza viungo wazuri achilia mbali handsball (henziboli )uliweza kutengeneza walinda milango bora na pia wapiga mashuti hodari ule mchezo wa kona uliweza kuzalisha wapiga vichwa hodari kama abeid Mziba (Tekelo )sasa viwanja vya wazihakuna pamerithiwa na miradi kama kumbi za vileo na makazi ya watu wenetu wanacheza game za luningani aah
Kweli MKUU

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom