Mr Alpha
JF-Expert Member
- Jul 31, 2018
- 273
- 765
Mshambuliaji timamu lazima pia uwe unabakiza pumzi ya akiba kwa ajili ya kufanya shambulizi la kushtukiza, tumeona Okrah na Mzize walipata nafasi ya counter attack wako wawili na beki mmoja wa mwisho engo tofauti lakini wakashindwa kutumia nafasi hiyo kwa kuzidiwa kasi na mabeki ina maana hawana uwezo wa ziada kufanya maajabu kwenye maeneo hayo ya mwisho.
Mwaka 2010 baada ya mshambuliaji Fernando Torres wa Hispania kufunga bonge la bao dhidi ya Ujerumani dakika za lala ulaliwe alihojiwa aliwezaje kufanya maajabu yale dakika mbaya ambazo kikawaida wachezaji wengi wanakuwa washachoka akasema yeye huwa anabakiza pumzi ya tukio maalumu iwapo ikitokea mpira uliokufa aweze kufanya shambulizi la kikatili kwa kasi ya ajabu kuwashinda mabeki wa upinzani. Jamaa alimlamba chenga beki kisiki Philip Lahm kisha golikipa Manuel Neur akalambishwa nyasi nyavu zikatikisika Hispania ikatwaa kombe la Euro.
Washambuliaji wote wa Yanga na simba wana tatizo hilo la ubutu, hawana uwezo wa kuamua mechi ngumu wakibanwa wanakuwa wa kawaida kabisa
Kama unafatilia soka la dunia utakubaliana nami mfano Didier Drogba aliyokuwa anafanya chelsea hata ile fainali ya UEFA mwaka 2012 ingekuwa hawa kina Mzize au Kibu Denis chelsea isingetwaa UEFA ile mbele ya Bayern Munich
Straika lazima uwe na kitu cha ziada usiwe yori yori
Hiyo ndio sifa inayowapa mishahara minono kina Karim Benzema, Luis Suarez, Haaland, Victor Boniphace nk