warumi
R I P
- May 6, 2013
- 16,218
- 18,440
Kwa mtazamo wangu tu,mi nadhani hao wanaohusika na mchakato mzima wa kuchagua nani aende BBA ingekuwa vizuri kama wangetushirikisha na sisi watanzani ambao kwa asilimia nyingi ndo tunahusika kwa kupiga kura na kumfanya mshiriki huyo ashinde,wazo ni hili,kwa wote watakaotaka kuchukua fomu za ushiriki ingekuwa vizuri ingekuwa open ili na sisi tupige kura na kuchagua nani aende na nani asiende,hiyo ingesaidia sana kwa washiriki kutoka tz kupigiwa kura kwa wingi coz tokea huku tuliwachagua wakatuwakirishe huko,au wao(BBA) ndo wanahusika kumchagua nani aende kutokana na vigezo wanavyotaka wao??,hili sijui.Hi kwangu mimi nadhan ingesaidia sana kuleta changamoto la shindano hilo,kwani siku zote naona washiriki wanaoenda uko inakuwa surprise kitu ambacho kinamfanya mtanzania kutokupiga kura kwa kuwa mshiriki huyo hakumpenda au hana mvuto kwake,hence washiriki wetu wote wanaambulia NOTHING BUT SHAME.Tofauti kwa ilivyokuwa kwa richard aliyejishindia mwaka 2007,yeye ilimlazimu kutumia akili nyingi za ziada kumfanya akubalike na kuwa mwenye mvuto wa kipekee mjengoni hali iliyomfanya nadhan kupigiwa kura hata na wasio watanzania wenzake,au alijitahidi kuji socialize na kuwa kivutio kikubwa mjengoni.Hali nahis haitakuwa nzuri kwa hawa washirik wa mwaka huu kutokana na haiba na muonekano wao wa kimagharibi gharibi yaani mashombeshombe hadi tabia haswa nando,watanzania wanapenda mtu social,asiyejisikia na mwenye haiba ya kawaida yaani kutokujisikia na kuonekana mjuaji saana.Hali ingekuwa shwali kama angeenda kwa mfano WEMA SEPETU,huyu mwanadada ana samu ya kukubalika sana na jamii hata muonekano na haiba yake ni ya upole na mwenye kuvutia mbele ya jamii,yaani ana nyota ya kipekee au mvuto kwa watanzania wengi,hayo ndo yalikuwa maoni yangu tu kuhusu shindano hilo la THE CHASE,otherwise wish the best for the contestant