Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Kamati ya maandalizi ya shindano la urembo nchini Ivory Coast (Miss Côte d’Ivoire 2025 -COMICI) imetangaza kuwa katika hatua za awali za mchujo, washiriki hawataruhusiwa kutumia nywele za bandia.
Badala yake warembo wote wanapaswa kuonyesha nywele zao za asili, iwe ni ndefu, fupi, au zimekatwa kabisa.
Kwa mujibu wa Victor Yapobi ambaye ni Rais wa COMITE MISS COTE D'IVOIRE - COMICI ambao ni waratibu wa shindano hilo, uamuzi huo unalenga kuhamasisha urembo wa asili wa Kiafrika na kuthamini uhalisia wa wanawake wa Afrika.
"Nywele za washiriki lazima ziwe za asili wakati wa hatua za awali za mchujo. Hakuna nywele za bandia. Hii inamaanisha kuwa rangi za nywele za kuongeza, nywele za kushonea, na mawigi haviruhusiwi," amesema Yapobi