Inside10
JF-Expert Member
- May 20, 2011
- 29,909
- 32,414
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imewahukumu Watanzania 64 kulipa faini ya Sh40,000 kila mmoja au kwenda jela miezi sita baada ya kupatikana na hatia ya kuondoka nchini kwenda Afrika Kusini bila kufuata taratibu za uhamiaji.
Walihukumiwa adhabu hiyo katika kesi ya jinai namba 31302 /2024 ni Abdallah Ramadhani, Abdul Rajab, Abdulrahman Mtimbe, Abdul Lusambi, Abubakary Kitemba, Ally Maduka, Adam Mkumba, Akida Ally, Ally Ally na wenzao 54.
Washtakiwa hao baada ya kuhukumiwa adhabu hiyo, walishangilia kwa kupiga makofi wakiwa ndani ya mahakama ya wazi namba moja, wakifurahia kupigwa faini ya Sh40,000.
Hata hivyo washitakiwa hao wamefanikiwa kulipa faini na kukwepa adhabu ya kwenda kutumikia kifungo cha miezi sita jela.
Hukumu hiyo imetolewa leo Jumatano Novemba 6, 2024 na Hakimu Mkazi Mkuu wa mahakama hiyo, Beda Nyaki baada ya washtakiwa kukiri kosa lao na mahakama kutiwa hatiani kwa kosa hilo.
Soma zaidi katika tovuti ya Mwananchi