Washukiwa wanne wa Al-Shabaab wauawa na Jeshi la Kenya

Washukiwa wanne wa Al-Shabaab wauawa na Jeshi la Kenya

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
1578031675079.png

Wanajeshi wa Kenya Alhamisi wamewaua washukiwa wanne wa wapiganaji wa kikundi cha Al-Shabaab na kumkamata mmoja wao baada ya tukio la kushambuliwa basi katika Kaunti ya Lamu.

Mratibu wa Mkoa wa Pwani John Elungata ametoa ripoti hiyo masaa kadhaa baada ya shambulio la kushitukiza katika eneo la Nyongoro, sehemu maarufu ambayo Al-Shabaab imekuwa ikifanya mashambulizi yanayo lenga abiria katika magari na vyombo vya usalama.

Watu watatu waliuawa na wengine watatu kujeruhiwa vibaya sana wakati washukiwa wa wapiganaji wa Al-Shabaab waliposhambulia basi lililokuwa linaelekea Lamu kutoka Mombasa.

Magaidi hao imefahamika kuwa walikuwa wanajaribu kulazimisha basi lisimame lakini dereva aliongeza mwendo, na hivyo ikawafanya walirushie basi hilo risasi.

Kamishna wa Kaunti Irungu Macharia amesema wale waliouawa na wengine waliojeruhiwa hawajaweza kutambuliwa hadi hivi sasa.
Timu za maafisa usalama zilipelekwa katika eneo la Nyongoro na maeneo yanayo lizunguka ili kukabiliana na wale waliowashambulia watu hao kwa bunduki.

Shughuli za usafiri zilisitishwa katika barabara ya Lamu-Garsen baada ya mabasi yaliyokuwa yanaelekea Mombasa kutoka Lamu na yale yanayo toka Lamu kwenda Mombasa yalilazimishwa kurudi Kituo cha Polisi cha Witu.


Chanzo: VoA Swahili
 
Hamna namna, ni kuendelea kuwaua tu na kuwawahisha huko wanakokwenda. Mashabiki wao humu JF habari kama hizi huwauma sana, haswa yule bibi kikongwe, siku hizi naona ametulia amechoka kujibizana na vijana JF....
 
Back
Top Bottom