Wasichana 98 wa miaka 10-19 huambukizwa ukimwi kila wiki nchini Kenya

Wasichana 98 wa miaka 10-19 huambukizwa ukimwi kila wiki nchini Kenya

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Wizara ya Afya ya Kenya imetangaza kuongezeka kwa kasi ya maambukizi ya ukimwi katika nchi hiyo. Wizara hiyo imeoa takwimu zifuatazo:

1650630323190.png

Chanzo cha Takwimu: Wizara ya Afya Kenya

Takwimu hizi za Wizara ya Afya kenya zinabainisha 98 wa miaka 10-19 huambukizwa ukimwi kila wiki nchini Kenya (Januari na Februari 2022). Kesi 45,724 za mimba za utotoni zilirekodiwa mnamo Januari na Februari ya mwaka 2022. Asilimia 21 ya mahudhurio yote ya kliniki za uzazi yalihusisha mabinti wenye umri kuanzia miaka 10-19 kwa mwaka (2021).

1650630455137.png

Chanzo cha Takwimu: Wizara ya Afya Kenya

Takwimu zinabainisha kuwa kesi 12,520 za unyanyasaji wa kijinsia na kingono ziliripotiwa nchini Kenya kwa mwaka (2021) ambapo katika kesi hizo, kesi 2,196 zilihusu wasichana wenye umri wa miaka 12-17 (Januari na Februari 2022). Wasichana 4,664 kati ya hao walipatiwa huduma za kuzuia VVU wakati 53 kati yao walikutwa na Virusi vya Ukimwi.

1650630806716.png

Chanzo cha Takwimu: Wizara ya Afya Kenya

Takwimu hizo zinaonesha kuwa Mikakati ya kupambana na Ukimwi nchini Kenya ilipunguza vifo vitokanavyo na Virusi vya Ukimwi kwa asilimia 67% kuanzia mwaka (2013 - 2021). Aidha, inaelezwa kuwa 83% ya watu wenye VVU nchini Kenya wanapokea na kutumia dawa za kurefusha maisha (ARV) mpaka mwaka (2021). Hii inamaanisha kuwa Watu wanaopokea dawa za kurefusha maisha walikuwa (600,000) mwaka 2013 na (1,200,000) mwaka 2021

Hivyo, kutokana na takwimu hizo ambazo zinaonesha ongezeko la maambukizi na unyanyasaji wa kingono nchini Kenya Serikali imeendelea kutoa wito kuundwa kwa sheria kali kudhibiti tatizo hilo sambamba na kuwataka wanajamii wa kenya wawe wamoja katika kuhakikisha wanapaza sauti na kudhibiti tatizo hili.
Nation Kenya
 
Njaa ndio sababu kubwa inayosababisha wasichana kujiingiza kwenye mapenzi kabla ya wakati
 
Njaa ndio sababu kubwa inayosababisha wasichana kujiingiza kwenye mapenzi kabla ya wakati
Sio njaa tu, bali tamaa na maadili mabovu na kulala kwa serikali zetu.

Inshort elimu ya ukimwi na matumizi ya condom kwa watu wa rika la miaka 15 - 22 imepuuzwa haka kageneration cha watoto wa miaka ya 2000's wanapigana miti mbichi-mbichi since day one,naamini wengi hawajui hata bei ya condom.

Hii ni noma kwa nchi nyingi za afrika ikiwepo sisi Tanzania.
 
Kwa kweli kuna vtu huwa vinanistikisha sana nikiskia mtu keshaanza ngono by 10years to 15yrs.

Kitu pekee ambacho mm huwa nakiona hapa ni malezi tu basi

Mm napenda ngono lkn sikuwahi kihivyo kutokana na pins zilizokuwa zimewekwa home na wazazi

So sad
 
Uneducated fools who don't understand the numbers already on the bandwagon. They obviously think the numbers are high and their country is better. lol.
 
Back
Top Bottom