Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Siku hizi wasichana wengi wazuri au warembo, ili kuwanasa, lazima uwahonge pesa nyingi.
Jamii imebadilika sana si kama zamani, ambapo mapenzi yalikuwa hayaangalii una pesa kiasi gani, mapenzi yalikuwa yanaangalia upendo wa dhati; yaani jinsi mtu anavyokupenda na malengo yake kwako.
Siku hizi msichana ukimhitaji kuwa naye kwenye uhusiano wa mapenzi, hata kama unaonana naye kwa mara ya kwanza barabarani, atakukubalia kwa maneno hapohapo na kukupa namba ya simu kama umemuomba.
Usidhani amekukubalia kwamba wewe ni mzuri sana au umemvutia kwa umbo au kwa maneno uliyompa, la hasha! Subiri dakika tu mkishapeana kisogo, halafu uangalie SMS zitakazoanza kuingia kutoka kwake.
Utakuta SMS kama baby naomba nisaidie pesa kidogo babu yangu anaumwa sana, nataka nikamuone kijijini, Tena anakuambia nitumie kwa simu, halafu maskini ya Mungu pengine babu yake anayesingizia anaumwa, alishafariki dunia miaka mingi iliyopita. Lengo ni kuanza kukulia pesa zako tu.
Ukishatuma hizo pesa za kwenda kumtazama babu yake, kesho utasikia naomba nitumie pesa kidogo nilikuwa ninadaiwa chuoni, sikumaliza ada!
Ukiona hivyo, ujue umeshakuwa mzazi wake, Rafiki nikuambie tu kwamba, kwenye mazingira kama haya, kuwa makini mno kwa sababu unaweza ukajikuta unapigwa pesa na kuambulia patupu!
Unachopaswa kujua ni kwamba, mwanamke huyo ataendelea hivyohivyo, akikuomba pesa ndogondogo hadi siku ya siku ambapo utashangaa imefika shilingi milioni moja, halafu ukimwambia mbona unazidi kuniomba pesa tu wakati sioni kama umenikubali kweli, utasikia atakachokwambia na utabaki umeduwaa.
yanayoendana na haya; “Vipesa vyako vinakuuma ehee! Kama vinakuuma nipotezee! Chukua time yako!”
Hapo hazungumzii kukurudishia pesa alizokula; yaani ameshakutenda, hapo utabaki unawaza bora hizo pesa ulizokuwa unamsaidia, ungefugia kuku wa nyama, pengine ungekuwa na biashara kubwa, ndivyo walivyo baadhi ya wanawake, hawana fadhila kwa wanaowapenda kwa dhati.
Dada yangu, mwanaume akikupenda, anaweza akawa anakula mkate na maji analala ili tu apate pesa za kukupa zitakazo-kuwezesha kufanya unachotaka.